Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga akiongea na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Mafinga Mji wakati wa baraza la kupitia hoja za CAG
Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga akiwa na mwenyekiti na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji wakati wa baraza la kupitia hoja za CAG
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji Happiness Laizer akiongea wakati wa baraza la kupitia hoja za CAG
HALMASHAURI ya Mafinga Mji imepogezwa kwa kupata hati safi miaka sita mfululizo kutoka kwa mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) ambayo imeendelea kuupatia heshima mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa baraza za kupitia hoja za CAG,mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga alisema kuwa kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano umepelekea halmashauri hiyo kupata hati safi.
Sendiga alisema kuwa baraza la halmashauri ya Mafinga Mji kwa kufanya kazi vizuri na ndio wamekuwa mfano kwa halmashauri nyingine za mkoa wa Iringa kuwa na uongozi bora na wenye ushirikiano.
Aliwataka watumishi wa halmashauri ya Mafinga Mji kuendelea kufanya kazi kwa kujituma kulingana na eneo ambalo analifanyia kazi.
Sendiga alimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji kuwachukulia hatua za kisheria kwa watumishi ambao wamekuwa wazembe kazini na kusababisha hoja za CAG.
Alisema kuwa haiwezekani kila wakati mtumishi anakuwa anasababisha hoja za CAG na hakuchukuliwi hatua yoyote na anaendelea kufanya kazi hapo hapo bila kuwajibishwa.
Sendiga alisema kuwa zilipatikana hoja 30 za mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) ambapo jumla ya hoja kumi na tatu (13) zimefanyiwa kazi na hoja kumi na saba (17) bado hazijafanyiwa kazi hivyo amegiza hoja hizo zifanyiwe kazi haraka iwezekavyo.
Aliongeza kuwa haiwezekani watumishi wawili ndio wachukuliwe hatua za kisheria wakati wengine wakiwa wameacha bila kuchuliwa hatua hivyo amemugiza mkurugenzi kuwachulia hatua za kisheria watumishi.
Sendiga alisema kuwa baadhi ya watumishi ambao wanahusika kukusanya mapato wamekuwa sio waamifu kwa kuwa wamekuwa wanazima mashine za kukusanyia mapato.
"Haiwezekani mashine inazimwa kwa zaidi ya siku 1000 haifanyi kazi na viongozi mpo hapo haiwezekani kabisa nakwambia mkurugenzi wachukuliwe hatua kali watumishi wanaosababisha kupotea kwa mapato ya halmashauri"alisema Sendiga
Alimazia kwa kusema kuwa matumizi yoyote ya fedha za halmashauri lazima yafuate utaratibu na kanuni zake ili kuhakikisha hazitokei hoja nyingine kwa CAG.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa Wanafanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato, ushirikiano mzuri,wanatoa mikopo, wanafanya vizuri kwenye uchumi kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano.
Mtambule alisema kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji amekuwa kiunganishi kikubwa baina ya wakuu idara na wafanyakazi wengine wa halmashauri kuwa kitu kimoja katika kufanya kazi.
Alisema kuwa ukatilii wa kijinsia bado upo wilaya ya Mufindi lakini wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara ili kuhakikisha wananchi wanajua madhara ya ukatili wa kijinsia na kupinga vitendo vyote ya ukatili.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji Happiness Laizer alisema kuwa wameyapokea maagizo yote ya mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga juu ya hoja za CAG na watayafanyia kazi ili kuhakikisha hawapati hoja nyingine mpya huku wakijitahidi kuzijibu na kuzimaliza hoja zote za CAG.