SHIRIKA LA UMEME TANESCOKUSITISHA HUDUMA ZA UNUNUZI WA LUKU KWA MUDA WA MASAA MAWILI

 Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema wateja wa huduma ya ununuzi wa umeme kupitia Luku watakosa huduma hiyo kwa saa mbili kwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi Juni 9 mwaka huu.

Huduma hiyo itakosekana kuanzia saa 6 usiku hadi saa 8 usiku nchi nzima ili kupisha maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wanaolipia kabla ya matumizi (Luku), kupitia mifumo iliyopo katika kituo cha kujikinga na majanga (Disaster Recovery).



Akizungumza  Juni 06/2022 kwenye makao makuu ya taasisi hiyo, Meneja Mwandamizi wa Tehama, Cliff Maregeli amesema kutokana na changamoto hiyo ya kiufundi wateja wanashauri kununua umeme wa ziada ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

"Maboresho ni muhimu na yanalenga kuongeza ufanisi kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme ili kuhudumia wateja wengi ipasavyo pale inapotokea hitilafu ya aina yeyote katika kituo chetu Kikuu Cha mfumo," amesema Maregeli

Kwa uapande wake Msemaji wa Shirika hilo, Martini Mwambene ameshauri wateja kuzingatia taarifa hiyo ili kuruhusu maboresho hayo ya mfumo kufanyika.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post