HALMASHAURI YA CHEMBA YADIRIA BILION 32.3 ZA BAJETI 2017\18
Na Woinde Shizza, Chemba
Halmashauri ya wilaya
ya Chemba imekadiria katika mpango wa fedha za bajeti yake kwa mwaka 2017/18
jumla billion 32.3 kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupokea mpango wa
Fedha wa mapato na matumizi ya
halmashauri zikiwa kama nakisi ya bajeti ya Halmashauri hiyo
Akisoma Taarifa ya
mpango wa mapendekezo ya Bajeti ya mwaka 2017/18 mkuruigenzi wa Halmashauri hiyo Semistatus
Husein Mashimba amesema kuwa pamoja na mapato na matumizi ya Halmashauri
inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukubwa wa eneo na ukosefu wa
usafiri wa ufikaji katika shughuli za kila siku hivyo kutofikia lengo. La makusanyo
yake na umaliziaji wa miradi kwa kasi.
Amesema kuwa bajeti
iliyopita wameitekeleza kwa asilimia 64% ambapo ya mwaka huu wa fedha hadi kufikia robo
ya pili wameitekeleza kwa 16% ikiwa ni bajeti ya mapato ya ndani ambapo
ametanabaisha kuwepo kwa changamoto mbali mbali zinazoifanya halmashauri hiyo
kushindwa kufikia lengo ikiwemo uchelewaji wa fedha kutoka serikali kuu,ukosefu
wa usafiri hususani magari huku halmashauri hiyo ikiwa na Km za mraba 7653.
Wananchi kuwa na Ari
ndogo ya uchangiaji wa mapato ya ndani kunakosababisha kutofikia malengo ya
maendeleo na mapato ambapo amemshukuru mh. Rais dkta John Magufuli kutekeleza
bajeti yao ya watumishi ikiwemo mishahara
yote kwa asilimia 100 na fedha zote za miradi ya maendeleo kwa mwaka huu 2017.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo Rajabu Omary akitoa hutoba wakati wa kufungua kikao hicho amewataka
madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kuwahasisha wananchi kuweza kuchangia
mapato ya ndani ya halmashauri hiyo kwani kimeshindwa kukidhi miradi ya
maendeleo na kushindwa kumalizika kwa wakati na hivyo kushindwa kufikia malengo
ya makusanyo ya ndani.
Amesema kuwa wajibu wao
ni kutekeleza majukumu yao bila kusukumwa na mtu na ndio msingi uwajibikaji
katika eneo lako la kazi na si kusukumwa na mtu huko ndio kunashindwa kuipeleka
mbale halmashauri yetu ambayo bado ni change na inahitaji watu sahihi wa kuendeleza
kwa moyo na uzalendo
Amesema kuwa pamoja na
ukosefu wa usafiri wa kufika katika maeneo mengi ya wilaya hiyo bado mpango wa
kuibua vyanzo vya ndani vya halmashauri hiyo itasaidia kuweza kufikia malengo
ya bajeti yao ya halmashauri naona kama kutakuwa na ufuatiliaji hii itasaidia
kufanikisha malengo ya bajeti yetu.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia