DIWANI WA CHADEMA AKUTWA ANAKESI YA KUJIBU

Kesi ya kutishia kuua inayomkabili Diwani wa kata ya Sekei kwa tiketi ya chama cha demokrasia maendeleo (CHADEMA)Chrispin Tarimo imechukuwa sura mpya baada ya mahakama kusema ana kesi ya kujibu.

Akitoa maamuzi ya kesi hiyo kama Diwani huyo ana kesi ya kujibu au la hakimu wa mahakama ya mwanzo Maromboso Vicky Makunguru alisema baada ya kusikiliza Utetezi uliotolewa na mashahidi Mustaph Munda,na Hamis Salehe wa upande wa malalamikaji katibu wa uenezi kata ya Sekei Sylvester Meda na mlalamikiwa Chrispin Tarimo kutokana na maelezo yao amegundua kuwa diwani huyo anakesi ya kujibu.

Hakimu Makunguru alienda mbali kwa kusema kuwa kutokana na maswali ya kudhalilisha aliyokuwa anatoa diwani huyo mahakamani hapo baada ya shahidi wa upande wa utetezi kusimama kutoa maelezo yake na kumtaka mlalamikiwa kutotoa kauli hizo.

Alisema hakimu Makunguru kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo  na upande wa utetezi umeonekana una uzito hivyo malalamikiwa atakuwa ana kesi ya kujibu na kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa mahakamani hapo dec 6 mwaka huu.

Nakumtaka diwani Chrispin  kuleta mashahidi mahakamani hapo siku hiyo kwa utetetezi kesi hiyo iliahirishwa hadi tar.6 dec mwaka huu.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post