Meneja wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungy akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi huo wa digital unaofanyika mkoani hapa kesho na unashirikisha wadau kutoka nchi za afrika
Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof.Makame Mbarawa anatarajiwa kufungua Mkutano wa Uzinduzi wa mfumo wa dijitali wa vyombo vya habari mkoani arusha kesho
Mkutano huo utawajumuisha wataalamu wa Jumuiya ya mawasiliano ya nchi za Afrika (ACRAN)ambao wataweza kufika Tanzania na kuzungumzia changamoto wa ubadilishwaji wa mfumo wa Analogi kwenda mfumo wa wa dijitali
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungy alisema kuwa mkutano huu umeratibiwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ambao utafanyika kwa siku tatu mjini hapa
Lengo la mkutano huu ni kuweza kufikia malengo ya ubadilishwaji wa mfumo wa Analogia kwenda Dijitali kwa nchi nzima na nchi wanachama wa ACRAN
Mkutano huu umekuwa ukifanyika kila mwaka nah ii ni mara ya sita na inashirikisha nchi ambazo ni wanachama ambapo Tanzania ni mara ya kwanza kufanyika mkutano huu na vikao vya bodi ya uongozi wa jumuiya hiyo imefanyika mara mbili hapa nchini
Pamoja na changamoto zinazoikabili mamlaka katika ubadilishwaji wa mfumo wa Analigia kwenda Dijitali Tanzania itaelezea mafanikio iliyoyapata katika utoaji wa elimu kuliko ukanda wa Afrika mashariki na itaelezwa mada katika mkutano huo juu ya utoaji elimu kwa umma juu ya mfumo wa digitali
Zaidi ya nchi 20 wanachama wa jumuiya ya mawasiliano wan chi za afrika wanashiriki mkutano huu na wanachama zaidi ya 150 kutoka nchi wanachama wamekwisha wasili tayari kwa mkutano huo
Pamoja na mengine Mungy alisema kuwa washiriki watapata fursa ya kutembela vivutio vya utalii ikiwemo mbunga ya wanyama ya ngorongoro