WAVAA MAGUNIA WAANDAMANA KUPINGA POSHO ZA WABUNGE


 picha ikionyesha diwani wa kata ya sombetini Alfonsi mawazo akiwa anongea na waandishi wa habari naye alikuwepo katika maandamano
wananchi wakiwa wamevaaa magunia katika maandamano ya kupinga posho ya wabunge


Wanaharakati wa kikundi cha wazalendo Assoca iate wamelazimika kutembea umbali wa kilometa saba kwa miguu huku wakiwa wamevaa magunia kwa shinikizo la kupinga posho za wabunge pamoja na maslahi ya wabunge kwa kuwa maslahi hayo yanalenga kumwangamiza mtanzania ambaye anategemea serikali.

Akizungumza mara baada ya kumaliza maandamano hayo mmoja kati ya viongozi wa kikundi hicho ambaye pia ni diwani wa kata ya sombetini akiwa amevalia vazi la magunia Bw.Aphonce Mawazo alisema kuwa wameamua kutembea peku pamoja na kuvaa magunia ishara ya kutoa taarifa kuwa muda si mrefu watanzania wote wataungana kuvaa vazi hilo kwa kuwa hawataweza kumudu gharama za maisha kwa ujumla

Bw.Mawazo alisema kuwa wameamua  kupaza sauti zao kwa wale ambao wamepewa dhamana ya kuwaongoza lakini badala yake ubinafsi umetawala hivyo hawako tayari kuona spika wa bunge Anna Mkinda na wabunge wake kujibinafsishia maliasili ya Tanzania kwa kukosa uzalendo.

Aliendelea kudai kuwa kitendo cha spika kusema kuwa wabunge wake wanaonekana ombaomba sio sababu ya msingi kwani kuna wananchi wengi wapo hapo Dodoma wanaombaomba kwanini wasiwasaidie.

,naomba kuuliza kuwa eti spika makinda anapodai kuwa eti wabunge wake ni ombaomba hivi hajawaona wananchi wa hapo Dodoma wakiwa wanaombaomba au kupanda kwa gharama za maisha ni mjengoni tu,,alisema mawazo

Aidha aliongeza kuwa hawatakuwa tayari kuona mbunge akiondoka bungeni na mil.12,gari lenye thamani ya milioni 94,posho ya laki mbili na nusu kwa siku ambo ni mshahara mfanyakazi muhimu kwa taifa  kama mwalimu,daktari,mwandishi wa habari,polisi na wengineo.
Pia ailisema kuwa pamoja nakuwa bunge la Tanzania linahadhi kubwa lakini lipo katikati ya wananchi maskini duniani lakini wabunge wake wanalipwa sawa na wabunge wa mabunge  yaliyoendelea duniani hali ambayo inaendelea kumkandamiza mwananchi wa Tanzania.

Kutokana na hilo Bw.Mawazo ailisema kuwa endapo kama bunge kupitia kwa spika Anna Makinda litaendelea kujadili posho,na maslahi yao bunge lijalo watalazimka kutembea kwa miguu huku wakiwa wamevaa magunia hadi Dodoma kwa miguu na kuhamasisha wananchi wengine nchi nzima mpaka bungeni Dodoma kama watauawawa basi ijulikane wazi wanapigania haki za watanzania.

Naye katibu wa wazalendo Associate John  Grayson  alisema kuwa Tuzo ya nishani aliyopewa Anna Makinda ni kwa ajili ya kutenda mema na kuwa mzalendo lakini ni kinyume na jinsi spika anavyofanya kwani anatetea ubinafsi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post