Ticker

6/recent/ticker-posts

MR.EBOO AZIKWA LEO ARUSHA MAELFU WAMIMINIKA

 Askofu Laizar kabla ya kuanza ibada
 dada wa marehemu Mr.Eboo akiwa anamuaga kaka yake
 familia ya Mr.Eboo ikiwa imekaa kwa uzuni wakati ibada ya mazishi ikiendelea
 Askofu Thomas Laizar akiw anauombea mwili wa marehemu Mr .Eboo
 watoto wa marehemu wakiwa na watoto wa dada za marehemu wameketi makaburini wakati mazishi yakiendelea
 Mke wa marehemu Mr.Eboo wa katikati akiwa analia kwa uchungu mara baada ya kuweka taji katika kaburi la mume wake
 mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiweka taji kwenye kaburi la Mr.Eboo
Maelfu ya wananchi ambao ni washabiki wa msanii wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava)Abeili Motika alimaarufu kwa jina la Mr.Eboo leo wamejitokeza nyumbani kwa mzee lotiko kuuaga mwili wa marehemu Mr. Eboo.

Wananchi hao ambao walikuwa na shauku ya kuuaga mwili wa marehemu huyo  walijitokeza wakionekana wakiwa na nyuso za masikitiko makubwa huku kila mmoja akihuzunika kwa kudai kuwa mwimbaji huyo wa bongo flava amewaachia pigo kubwa kwani alikuwa anaelimisha jamii kwa kupitia nyimbo zake.

Akiongea katika mazishi ya msanii askofu mkuu wa jimbo la kaskazini Thomasi Laizer alisema kuwa wao kama kanisa wameupokea msiba huo kwa masikitikio makubwa kwani msanii huyo alikuwa anaelimisha jamii kupitia nyimbo zake pia aliweza kuutangaza mkoa wa Arusha pamoja na kabila la kimasai kupitia nyimbo zake .

Alitoa wito kwa wananchi ambao ni vijana kuiga njia ambazo msanii huyo alikuwa anafanya na kuenzi nyimbo zake pamoja na kuendeleza taaluma yake ya uimbaji katika jamii .

“sasa nyie mliobaki husasa ni vijana ajira sio mpaka muajiriwe bali mnaweza mkabuni mwenzenu Mr Eboo alikuwa ajaajiriwa na mtu bali alikuwa amejiajiri yeye akwenda chuoni lakini nyimbo zake ndo zimefanya mpaka hata nyie wenyewe mkaja kumzika “alisema Laizer

Aidha alibainisha kuwa anapenda kuwasihi wamasai ambao bado wanaendeleza mila za kwenda kumtairi mwanamme kwa nguvu akiwa mtu mzima waziache kwani hazina faida kwa sasa kwani wanaweza kupata hata mathara kupitia njia hiyo na badala yake wamgeukie mungu.
Msani huyo amefariki dunia  saa  katika hospitali ya dream seminari inayomilikiw ana kanisa katoliki lililopo Usa river Wilalyani Arumeru mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili Nyumbani kwa baba wa marehemu kaka wa msanii huyo Olais Loshila Motika alisema kuwa marehemu Mr.Ebbo alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kansa ya ngozi na aliwashukuru watu wote ambao walishirikiana nao katika safari hiyo ya mwisho ya mrEboo..

Alisema kuwa marehemu alisumbuliwa na ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi tisa ambapo kabla ya kuumwa alikuwa anaishi mkoani Tanga na alipozidiwa aliletwa mkoani hapa kwa ajili ya matibabu na aliwahi kutibiwa katika hospitali nyingi ikiwemo Mounti meru ,KCMC pamoja na hospitali ya kanisa ya seliani.

Aidha alibainisha kuwa marehemu Mr.Ebbo ameacha mjane na watoto watatu wote wakiwa ni wakike


Libeneke lilizungumza na mmoja wa washabiki wa msanii huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Ally Abdi alisema kuwa amepokea msiba huo kwa masikitikio makubwa sana kwani alikuwa anampenda msanii huyo sana na alisema kuwa anafurahishwa na kibao acha boda boda ambacho msanii huyo alikiimba kabla ya kuanza kuumwa.

Post a Comment

0 Comments