watoto wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa megatrede waliowatembelea katika kituo cha Samarisani
Meneja masoko wa MegatredeMahaligewi Elinawe akimkabithi mtoto george msaada wa madafrari
Meneja masoko wa Megatrade akiwa anamkabidhi msaada mratibu wa kituo cha kulele watoto yatima waishio na virusi vya ukimwi cha St.Lusia John Shemzigwa wakati walipowatembelea kituo hapo.
wafanyakazi wa megatrade wakiwagawia watoto juice na soda
KAMPUNI ya megatrade ya mjini hapa imekabidhi msadaa wa
vyakula venye thamani ya shilingi milioni tatu kwa watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi
(HIV ) ambao wanaishi katika mazingira magumu wa kituo cha kulele watoto cha
St.Lusia kilichopo Njiro jijini hapa .
Akikabidhi msaada huo meneja wa kampuni hiyo Mahaligewi Elinawe alisema kama kampuni
ya megatrade alisema kuwa ni kawaida yao wakati wa msimu wa sikukuu kama huu
kuwakumbuka watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu haswa wakiwa ni
watoto yatima na watoto ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi .
Alisema kuwa wao kama megatrede waliamu kutoa msaada huu wa
vyakula kama hivi ili kuweza kuwaweka watoto hawa katika hali ambao na wao
watajisikia wapo kama watoto wengine ambao
wanawazazi wao.
Alisema wao wanapenda kushirikiana na jamii katika kila
jambo ambapo wameona ni vyema wakijumuika nao katika sikuu hizi ili na watoto
nao wajisikie wapo kama wanawazazi na alisema kuwa anapenda kuwaomba watanzania
pia wajitokeze kwa wingi kusaidia watoto wa namna hii kwani kutoa ni moyo na
sio utajiri.
“pia napenda kuwasihi wakina mama na wakina dada ambao kwa
wakati mmoja au mungine wanajikuta wanakuwa na familia zao waweze kuwalea
watoto wao katika familia zao na wajirudi waweze kukaaa na watoto wao wakiwa
wamewazaa na sio kuwatelekeza ovyo hali inayosabibisha ata ongezeko la watoto
wa mitaani iwapo hawatapata wafadhili wa kuwasaida’alisema Elinawe.
Alitoa wito katika jamii na kusema kuwa muda wa
kuwanyanyapaa watoto umepitwa na wakati watu wanataka kiwa kukaa na watoto hawa
kama watoto wengine wowote wale na pia napenda kuwasihi watanzania waendelee
kuwakumbuka watoto hawa ambao wanaishi na virusi vya ukimwi kwani wao sio
yatima tu bali ni wanaoishi na virusi vya ukimwi .
Alisema kuwa muda wa kunyanya paa watoto umeisha wanatakiwa
wakae na watoto hawa vizuri kama watoto
wengine kwani hawakupenda kuwa ivyo hivyo wanaoishi majumbani walioko ivi
tunatakiwa kuwapenda na kuishi nao bila ubaguzi wowote.
“napenda kuwasihi watu wengine wajitokeze kuwasaidia watoto
hawa kwani wanaishi katika mazingira magumu sana na wanaitajika mahitaji mengi
zaidi kwani watoto hawa ni waadhirika hivyo wanaitaji uduma nyingi kama chakula
cha kutosha mbogaa mboga na vingine vingi hivyo wananchi wajitokeze kusaidia
watoto kama hawa wanaoishi na virusi vya ukimwi wa St,Lusia”alisema Elinawe
Akipokea msaada huo Mratibu wa kituo St.Lusia kituo ch
akulelea watoto yatima wanaoishi na virusi vya ukimwi John Shemzigwa alisema
kuwa amefurahishwa sana na ujio wao wa kutembelea watoto hao ambao ni watoto
yatima ambao wametelekezea na wazazi wao na wanaishi na virusi vya ukimwi.
Aidha alisema kuwa mazingira ambayo watoto wanaishi ni
mazingira magumu mno ukizingatia watoto wanaishi na ugonjwa wa ukimwi lakini
wao kama kituo wamewakusanya na kukaa nao vizuri ili nao wajisikie wapo kama watoto wengine ikiweomo kuwasaidia kuwapa dawa
pamoja na kuwapa mahitaji yote ambayo mtoto anatakiwa kupewa.
Alisema kuwa wao kama ST.Lusia wanapenda kuwasihi mashirika
mengine wajitokeze kusaidia kituo hichi kama
shirika linaloangalia watoto hawa.
“Aliwaasa Wanawake haswa vijana ambao wanabemba mimba wakiwa
mashuleni waache kutupa watoto kwani watoto hao ni mawaziri wa baadaye ma raisi
wa baadae hivyo wawalee na sio kuwatupa’’alisema Shemzigwa.
Alisema kuwa wanakutana na changamoto mbalimbali za kuwalea
watoto hawa ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwahudumia watoto hawa kipindi
wanapokuwa wanaumwa.
Aliiomba serekali na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi kusaidia watoto hawa pia aliiomba serekali iwasaidie kuchimba kisima cha
maji ambacho kitawasaidia wao kupata maji kwani wamekuwa wanapata shida sana ya maji hali ambayo
inawashinda hata kulima mboga mboga kwa ajili ya watoto hawa.
‘napenda kuomba watusaidie japo kuchimba maji kwani tunakosa
hata namna ya kulima mboga kwa ajili ya watoto hawa kwani hatuna maji maji hapa
kwetu ni yashida sana
hivyo tunaomba watusaidie ili tuweze kuwalimia japo mboga ambazo watakula
ziwaongezee kupandisha cd4 zao”alisema Semzigwa.
Kampuni hii ya megatrade ili toa msaaada katika vituo viwili
vya kulele watoto yatima ilitoa katika
kituo cha St.Lusia kituo ambacho kinalelea watoto wenye virusi vya ukimwi
pamoja na kituo cha Samarisani ambapo
wametoa msaada wa vyakula ikiwemo unga,Mchele ,mharage mafuta ya kupikia
,juice,sabuni ,Biskuti madafutari ,chakula ya lishe kwa ajili ya watoto wadogo
pamoja na pamoja na sabuni .