SEREKALI YATAKIWA KUKARABATI MLIMA KILIMANJARO

kazana bwana twende tumalize

Tima akiwa anakunywa maji wakati wakiwa wampumzika njiani
Tima akiwa na msadizi wake akipanda mlima
Hali ya hewa ya mlima kilimanjaro ilivyo uko juu
Tima na Alex wakiwa mlimani sehemu ya kula
Msafara ambao ulipanda mlima kilimanjaro uliokuwa umeongozana na watoto wa Brigedia Nyirenda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kurejea

Tima akiwa na kaka yake Alex wakiwa wanashuka ngazi kwa ajili ya kuondoka mara baada ya kutoka mlimani

asante mungu nimefika alisema Tima

Serekali kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya wanyamapori Tanzania (TANAPA)wameombwa kuboresha mazingira ya mlima kilimanjaro  ili watalii pamoja na wazawa wanaoenda kupanda mlima huo wasipate shida.

Hayo yalibainishwa na mtoto wa aliyekuwa brigedia wa kwanza kupandisha mwenge wa uhuru katika mlima kilimanjaro  Nyirenda Alex wakati alipokuwa akiongea na gazeti hili mara baada ya kushuka mlimani.

Alisema kuwa hali ya mlima ni nzuri lakini kuna vitu ambavyo vinapaswa kuboreshwa zaidi ili kuweza kuongeza wageni wanaotembelea mliama wetu .

Alibainisha kuwa moja ya vitu ambavyo serekali na Tanapa inatakiwa kujenga ni pamoja na sehemu ambayo watalii watatumia kupata chakula kwani wamekuwa wakipata tabu sana wakati wakila.

"unajua kiukweli mlima wetu ni mzuri vyoo ni vizuri ila kunatatizo moja hamna sehemu nzuri ya kula chakula na ukiangali huko juu mlimani kunanyesha mvua kila siku sisi juzi tulivyopanda ilifika mahali tukashindwa kula ata chakula cha mchana maana mvua inavyesha hamna sehemu ya kujifiicha ili tupate chakula kwakweli ni jambo lakusikitisha sana na ukilinganisha na hela ambayo serekali inapata kupitia mlima huu"alisema Alex.

Alibainisha kuwa katika miaka 20 iliyopita ambayo walipanda mlima huo kulikuwa na sehemu ambazo kipindi hicho watu walikuwa wanakoka moto ule mda wa kula au wakukutana kupata chakula wanaota lakini kwa sasa hamna hivyo aliiiomba serekali ijaribu japo kurudisha mfumo wa zamani wa kukoka moto ili angalau wageni wanaopanda mlima huo waweze kupunguza baridi kupitia njia hiyo na pia alisema iwapo watafanya hivyo watawaongezea wageni kwani kuna wageni ambao hawajawai kuona moto kama huo unawashwa msituni hivyo itakuwa ni kama miujiza kwao.

Alitoa wito kwa watanzania kujijengea tabia ya kutembelea mlima huo kwani upo kwao na nikitu cha maajabu sana kinachofanya adi wageni wanakuja kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuuona mlima huo tu.

"mimi kwakweli napenda kuwasihi watanzania wawena moyo wa kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini kwani na vya kwao wenyewe ,kwanini watu wanatoka nje ya nchi wanakuja kuangalia wao wenyewe wapo hapa hawataki kuja kuangalia kwakweli wawe na moyo wa kutembelea"alisema Alex

Kwa upande wa dadake Tima Nyirenda alisema kuwa anashukuru mungu wa sana kwa kupanda mliama huo ambao wao kwao ni historia kubwa na kumbukumbu kubwa ya baba yao mzazi ambaye alipandisha mwenge wa uhuru katika mliama huo.

Alisema kuwa wao walipanda mliama huo lakini hawakuweza kufika katika kilele ambacho ambacho baba yao alifika kwani kutokana na hali ya hewa iliwakwamisha ila aliaidi kuwa kwa kuwa huu ni mwanzo wanaamini kabisa katika kipindi kijacho cha mwaka ujao watafika kileleni .

"kwakweli tulikuwa tunahamu sana ya kufika katika kilele ambacho baba alifikisha mwenge wa uhuru enzi izo katika miaka ya 1961 lakini hatukufika tuliishia kibo ambapo tuliweza kutembea kilometa 4750 na katika mlima kilimanjaro mfano tungefika kileleni tungetakiwa tutembee kilometa 5685  kwa iyo tumebakiza kilometa 935 tu hivyo nathani mwaka ujao tutamaliza maana hii tumeanzisha mpango wa watoto wa Gwebe  Nyirenda kupanda mlima kila mwaka"alisema Tima

Aliwataja watu ambao walikuwa nao katika kikundi chao cha kupand amlima huo waliomaliza kuwa ni rafiki wa babake Ameen Kashimiri,Rahimu Kashimir ,Paul Mason pamoja na Lorly Lavilla.

Alitoa wito kwa watanzani kujenga tabia ya kupanda mlima huo ambao ni kivutiio kikubwa duniania .


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post