mbunge wa viti maalum kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi mery chatanda akiwa anampa mkono mkuu wa mkoa wa Arusha mstaafu Isdori Shirima katika sherehe za kumuaga mkuu huyo wa mkoa na kumkaribisha mkuu mungine wa mkoa Magesa Mulongo
Kamati ya ulinzi na usalama ikiwa inapeleka zawadi kwa mkuu wa mkoa mstaafu
walijitokeza wengi katika sherehe hizo za kumuaga mkuu wa mkoa na kumkaribisha Mulongo
kulikuwa na viongozi wengi waliouthuria katika sherehe hizo hapo ni baadhi ya viongozi waliokuwepo meza kuu
Mrs Magesa Mulongo akiwa anapokea zawadi ya kukaribishwa katika mkoa wetu
Mkuu wa mkoa Isdori Shirima alipewa mbuzi kwa ajili ya maziwa
mkuu wa mkoa wa mstaafu aliyoko kushoto Isdori Shirima akiwa anapokea zawadi kutoka kwa mkuu wa mkoa wa aliyemuachia madaraka Magesa Mulongo katika sherehe hizo zilizofanyika katika hotel ya Kibo pallace mkoani hapa
MKUU wa mkoa
wa Arusha,Magesa Mulongo amesema kuwa yeye kama kiongozi wa mkoa atahakikisha
anakufa au kupona kwa lengo la kuhakikisha mji wa Arusha unakuwa na amani na
utulivu.
Aidha mkuuu huyo amewataka
viongozi mbalimbali wa dini mkoani hapa waache mara moja tabia ya kuitukana
serikali iliyopo madarakani na badala yake waiombee kwa madai kuwa hakuna aliye
mkamilifu duniani.
Mulongo,alitoa
kauli hiyo katika hafla ya kumuaga mkuu wa mkoa mstaafu wa Arusha,Isdori
Shirima sherehe iliyofanyika katika hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoani hapa.
Alisema kuwa
yeye kama kiongozi mkuu wa mkoa wa Arusha atahakikisha wakazi wa Arusha
wanalala na kuamka salama bila matatizo huku akisema ya kuwa amani katika mkoa
wa Arusha ni muhumi katika kipindi hiki.
“Kwa hili la
amani na utulivu lazima nitakufa nalo,lazima watu walale na waamke salama”alisema
Mulongo
Alisisitiza ya kuwa wadau mbalimbali katika
mkoa wa Arusha wanajukumu la kuhakikisha mkoa wa Arusha unakuwa kimbilio la
watu wa kada tofauti wakiwemo wastaafu .
Alisema kuwa
wakazi wa Arusha kamwe hawawezi kula siasa bali wanatakiwa wale maendeleo na
kuvisisitiza vyama vya siasa majina ya vyama hivyo yasiwatenganishe.
“Watu wa
Arusha hawawezi kula siasa wanahitaji maendeleo nawaomba tushirikiane na tuifanye
Arusha kuwa kimbilio la wanyonge kama wastaafu na Arusha ni yetu sote”alisisitiza
Mulongo
Hatahivyo,alihaidi
kuwapa ushirikiano mzuri wafanyabiashara,wanasiasa na makundi mbalimbali ya
kijamii huku akiwataka wawe wa kwanza kusisitiza na kutangaza amani mkoani
hapa.
Naye,mkuu wa
mkoa mstaafu wa Arusha,Isdori Shirima aliwaomba radhi wakazi wa Arusha ambao
aliwakosea katika kipindi cha uongozi wake huku akisema kuwa hata yeye
amewasamehe wale wote waliomkosea.
Alitoa wito
kwa viongozi mbalimbali mkoani hapa kuhakikisha wanawatumikia wananchi
waliowapa dhamana huku akisisitiza kuwa endapo katika kipindi chake udhaifu ulijitokeza
lakini ni tabia ya binadamu.
“Katika
kipindi change huenda niliwakwaza watu lakini ni udhaifu wa mwanadamu,nawaomba
radhi wale wote niliowakosea lakini hata mimi nimewasamehe kwani kinyongo
huongoza nyongo”alisema Shirima
Katika hafla
hiyo halmashauri ya wilaya ya Karatu ambayo inaongozwa na upinzani ilivuta
hisia za watu pale mwenyekiti wake,Lazaro Maasaye alipoamua kumkabidhi zawadi
ya ndama Shirima kutokana na mchango wake,huku ikimwagia sifa kiongozi huyo kwa
kudai kuwa pamoja na halmashauri yao kuongozwa na upinzani lakini kiongozi huyo
hakujali itikadi za kisiasa.