WATAKIWA KUFUATA SHERIA

 Viongozi  waliokutana katika mkutano wa taasisi zinazosimamia na kuthibiti ubora wa elimu

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Philipo Mulugo amewataka wadau wa elimu kutunga sheria kali na kuipeleka wizarani ili vyuo vinanavyoisumbua serikali hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Taasisi zinazosimamia na kuthibiti ubora wa elimu Tanzania uliofanyika mkoani hapa.

Mulugo amesema kuwa ili serikali kupitia wizara yake iweze kuviwajibisha baadhi ya vyuo vikuu ambavyo havifuati taratibu na vimekuwa vikiisumbua serikali ni lazima sheria kali itungwe ili wahusika waweze kubanwa.

Aidha mulugo ameongeza kuwa mkutano huo ni muhimu sana kwa kuwa Tume ya vyuo vikuu(TCU)ndio waandaji na wamewakutanisha taasisi za elimu ya juu ambapo amewataka kujadili changamoto zote zinazoikabili elimu na kuhakikisha kuwa elimu inakidhi mahitaji ya soko la pamoja.

Waziri amesema kuwa ni lazima umakini wa hali ya juu utumike kwenye shule za Tanzania ili watoto wanaopata elimu hiyo waweze kuwa na vigezo vya kuingia katuika soko la ajira.
Hata hivyo amelitaka jukwaa hilo kujadili tatizo la walimu ngazi zote kwa kina na sio kuongeza walimu tu bali njia mbadala ya ya kumfanya mwalimu wa Tanzania kuipenda na kujivunia kazi yake.

Pia amesema lugha sahihi ya kufundishia inayotakiwa  pamoja na tatizo sugu la migomo ya shule na vyuo  ambapo amesema kuwa ongezeko ni kubwa na mingi inahusiana  na taaluma hivyo amewataka kubaini chanzo chake ili njia mbadala ya kutatua ipatikane.

Vile vile amelitaka jukwaa hilo kujadili gharama za masomo kwa vyuo vikuu sanjari na shule ambapo amesema zimekuwa kubwa sana hivyo njia mbadala itafutwe ili kuhakikisha kila anayehitaji amnaweza kumudu.

kwa upande wa matokeo ya darasa la saba alisema kuwa kutokana na matokeo ya mwaka huu kuja na kuonyesha wanafunzi wengi wamefanya udanyanyifu kwa kusudia hivyo watachukuliwa hatua hata walimu ambao walihusika na kitendo hicho cha kuonyesha wanafunzi mitiani na alibainisha kuwa kwa kama mwalimu mkuu wa shule atabainika kuwa yeye kahusika na tukio hilo atashushwa cheo na ikiwezekana ataamishwa kituo kabisa.

"unajua uwezi kusema mwanafunzi wa darasa la saba ajui jema au baya nikweli alikuwa ajui kuibia au kuonyesha mtiani ni vibaya wanajua wale ni watu wazima wanaakili hivyo lazima wachukuliwe hatua ili iwe fundisho "alisema mulongo

Naye katibu mtendaji tume ya vyuo vikuu Profesa Sifuni Ernest Mchome amesema kuwa mkutano huo unalengo la kujadili changamoto zinazowakabili na kuhakikisha kuwa elimu inayopatikana  ni bora na inakidhi malengo waliyojiwekea.

MCHOME amezitaja baaadhi ya taasisi zinazosimamia na na kuthibitio ubora wa elimu zilizoshiri mkuwa ni pamoja na Tume ya vyuo vikuu,baraza la taifa la elimu ya ufundi staidi,mamlaka ya elimu ya ufundi stadi,baraza la taifa la mitihani,bodi ya mikopo ya elimu ya juu,mamlaka ya elimu Tanzania,taasisi ya elimu Tanzania.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post