Meneja wa Magic Fm Dativus Mango(kushoto) akifafanua kuhusu kuvunjika kwa shoo ya mwanamziki Fally Ipupa (katikati)kulia ni meneja wa mwanamziki huyo Madina Djo Boungue
.Mkurugenzi wa Mtongee Klabu Somyo Lebi
SHOO ya mwanamziki nguli kutoka Kongo Pally Ipupa iliyokuwa ifanyike,mwishoni mwa wiki (Ijumaa) katika ukumbi wa Matongee jijini Arusha,imevunjika na kusababisha vurugu kubwa kutoka kwa mashabiki kuleta fujo wakitaka kumpiga mwanamziki huyo na waandaaji , kupora vitu mbalimbali ikiwemo viti na fedha za kiingilio.
Hatua hiyo imetokana na uongozi wa klabu ya matongee kuwa na maandalizi mabovu ikiwa ni pamoja na kushindwa kulipia jenereta la uhakika na kuleta jenereta bovu la bei ya chini lililoshindwa kuzalisha umeme wa kuendesha vyombo vya mziki vya mwanamziki huyo nguli.
Kwa mujibu wa meneja wa Radio Magic ,Dativus Mango ambao ndio waandaaji wa Shoo hiyo,alisema shoo hiyo imevurugika na kushindwa kufanyika kutokana na sababau ya umeme kuwa mdogo ,ambapo uongozi wa Ukumbi wa Matongee ulishindwa kutofanya maandalizi ya kutosha ikiwemo kutafuna Jenereta la kukabiliana na tatizo la Umeme .
Akiongea na waandishi wa habari,Mango alisema kuwa Shoo hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya kusherehekea miaka miaka 50 ya uhuru sanjari na kutimiza miaka 10 kwa kituo cha radio cha Magic Fm.
Alisema kuwa wamepata hasara kubwa ikiwa ni pamoja na kulipia ukumbi shilingi milioni 1.2,malipo ya kumleta mwanamziki huyo ambayo ni Euro 25,000 sawa na fedha za kitanzania sh,milioni 50 na gharama zingine kibao.
Nae Fally Ipupa alisema kwamba amesikitishwa sana na kitendo hicho kwani amedhalilishwa sana na mashabiki kwa kutukanwa matusi na akatumia nafasi hiyo kuwalalamikia waandaaji wa onyesho hilo .
Fally alieleza kwamba ameonekana kama tapeli kwa wapenzi wa mziki wake hapa Arusha kwani ametumia masaa matano kutoka Nigeria kwa ajili ya kuja Arusha kufanya shoo ya nguvu na kusisitiza kwamba hakupenda kuona mashabiki wakitoa kiingilio bila kuona shoo yake.
Akizungumzia adha hiyo mkurugenzi wa matongee klabu,Sombyo Lebi alisema kuwa mara baada ya kufunga vyombo vya mziki umeme ulikuwa mdogo na kuanza jitihada za kutafuta jenereta lingine na ilipofika majira ya saa 5 usiku mashabiki walianza kupiga kelele wakitaka warudishiwa viingilio walivyolipia mlangoni sh,15,000.
Pamoja na jitihada za kupata jenereta lingine mashabiki hao walianza kufanya fujo ikiwemo kubebe viti na kusababbisha upotevu wa viti 1700 na uharibifu wa vitu mbalimbali.
Mbali na hapo Libeneke liliweza kushuhudia mashabiki wakibebana na viti kila mmoja akionekana akiwa na amebeba viti kuanzia vitatu kupanda juu na wengine kubeba hata viti saba na katika mashabiki hao kuna baadhi waliikuwa wakiviuza viti hivyo usiku huo huo huo kwa bei ya shilingi 6000 kwa kila kiti kimoja .