Ticker

6/recent/ticker-posts

MVUA KUBWA ILIVYOSABABISHA MAAFA KARATU MKOANI ARUSHA

Lori la mizigo lenye namba T190 AKW lililokuwa limebeba mitambo ya kutengeneza barabara likitoka Engaruka kwenda Arusha likiwa limezama kwenye maji.
 Baadhi ya magari yaliyokumbwa na mafuriko hayo

Hakika maafa yatokeapo hukumba kila kiumbe hai katika jamii. Mbwa huyu si kuwa aliathirika na mafuriko hayo bali alionesha uzalendo wake wa kweli na kufika katika eneo la tukio na kuangalia mwenyewe kilichojiri.
Mfanyakazi wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Augustino Masige, aliyekuwa akiendesha gari namba T573 AHW, akitoka Arusha kwenda Musoma, akisimama kando ya gari lake lililosukumwa na maji umbali wa mita 50 toka barabarani.
 
Mwili wa marehemu Samweli Julius ambaye alikuwa ni msaidizi wa mitambo ya kutengeza barabara, ukiwa umenasa juu ya mti
Baadae polisi wakatoa idhini ya mwili wa Samweli kutolewa katika eneo ulipopatikana.

Hivi ndivyo kipande hicho cha barabara kilivyomegwa na maji.
  Polisi walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi wa matukio hayo ya ajali.
Wananchi wakishuhudia maafa yaliyosababishwa na mafuriko hayo.

Post a Comment

0 Comments