No title

Serekali imetoa tamko la kukahakisha kuwa kila mtanzania ambaye ni mtazamaji wa Televison hapa nchini ambao wanatumia huduma za vingamuzi wanavipata  vingamuzi hivyo kwa gharama ndogo  ambavyo vitawezesha wananchi kupata unafuu wa huduma za vingamuzi.

Tamko hilo limetolewa  na Naibu Waziri  wa  Mawasiliano ya sayansi na Teknolojia  Charles Kitwangwa Wakati akifungua mkutano  wa sita wadau wa mawasiliano nchi za Africa iliuofanyika jijini Arusha na kuratibiwa na mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA.

Naibu waziri huyo amesema kuwa ingawa kwa sasa hivi zipo takribani kampuni Tatu zilizoruhusiwa kutoa huduma za vingamuzi hapa nchini ambapo kimtazamo zinaleta mchanganyo kwa wanachi ipi watumie na ipi waache na sio rahisi kwa manachi kununua vingamuzi vyote vitatu .

Katika kuona hilo Naibu waziri  Charles  Kitangwa amesema kuwa wapo mbioni kukaa na kampuni hizo tatu na kupanga na kupata njia bora ambayo haitampa mzigo mkubwa mwanachi  kwa kuangalia jinsi vingamuzi hivyo vitakayo wea kuboreshwa sambamba na kushushwa bei.

 wageni nao walikuwepo
 wafanyakazi wa TCRA wakiwa wamevalia sare zao wakasikiliza wakati mkutano unaendelea
Naibu Waziri  wa  Mawasiliano ya sayansi na Teknolojia  Charles Kitwangwa akiongea katika mkutano huo


Mkutano huu ambao umeandaliwa na TCRA  ambao ni wasiku tatu amelenga kuangalia kwa undani changamoto ambazo nchi za Africa ziankabilaina nazo katika kujiingiza katika mfumo wa kidigital , ikiwa vyombo vya Tanzania viepewa ukomo mpaka mwaka 2013.


"mkutano huu wakutana kuangalia  jinsi nchi za afrika zitashirikiana kuangalia kwamba wale ambao wameshaingia kwenye mfumo wa kutumia digitali waweze kutoa uzoefu wao kwa wale ambao wapo nyuma na pia haiwezekana kwenda kwenye digitali bila kuwa na maandalizi ya awali ukilinganisha kuwa nchi yetu kama Tanzania inachukuwa uwenyekiti"alisema Kitwangwa.

Alibainisha kuwa serekali mpaka sasa hivi haina mpango wa kumuwezesha mtu ambaye ana uwezo wa kutumia kimwaguzi hicho ila wapo katika majadiliyano ya kuona namna gani wanaweza kupunguza bei hii na majadiliyano hayo yapo baina ya TCRA na TRA ambapo wataangalia kama itawezekana kuondolewa kwa ushuru katika vifaa hivi .

Alitoa wito kwa watanzania  husa ni wafanya biashara katika kipindi hichi cha kuhama kutoka  kwenye adologia kwenda kwenye digitali hivyo kila mmoja anaenda kununua kifaa dukani aulize kabla ya kununua Tv hiyo kama ni adologia au digital .

" napenda kuwaambia watanzania wanaoenda kunua hivi vitu madukani waulize kwanza kabla ya kununua na pia wauzaji wasidanganye wanunuzi wawape ukweli kwani nimeshasikia pia vitu hivi vimeanza kushushwa bei hivyo watanzania wawe makini"alisema Kitwagwa.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post