BREAKING NEWS

Friday, December 23, 2011

KIMOTOROK WALALAMIKIA TANAPA ,TANAPA WASEMA SISI SIO WAVAMIZI WA MAENEO


Kaimu mkurugenzi muhidhi Mtokonologia ,Idara ya Ikologia Jastini Muhando akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana shutuma za mgogoro huo 



Wanakijiji wa kijiji cha Kimotorok wamemuomba rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete kuwafukuza kazi haraka waziri wa maliasili na utalii Ezekiel maige pamoja na mkurugenzi mkuu wa TANAPA  Alan Kijazi kwa kitendo cha kuzidi kuzorotesha mahusiano kati ya serekali yake na vijiji lvinavyopakana na hifadhi za taifa.

Wananchi wa  halmashauri ya kijiji cha kimotorok kilichopo Orkessumet wilayani Simajiro mkoani Manyara wamefikia hatua hiyo kutokana na unyanyasaji wanaoupata kutoka katika  mamlaka ya hifadhi ya taifa TANAPA kwa kitendo cha kuvamia aridhi ya wafugaji kwa nguvu na kuwataka waondoke ili kupanua hifadhi ya Tarangire National Park.

Wakiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa serekali ya kijiji ya kimotorok Daniel kunyae Melau alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikiwanyanyasa wanakijiji wa eneo hilo hali iliyofanya wanakijiji hao kuishi kama digi digi.

Alisema kuwa mamlaka hiyo kupitia askari wake wa ulinzi imekuwa ikiwafanyia vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kuchoma moto nyumba zao  ,kuwapiga wanakijiji pindi tu wawawaonapo katika maeneo hayo.

"askari hawa wa Tanapa wamekuwa wakitufanyia vitendo vya kinyama sana ma tunaushaidi wa kutosha  kwani mnamo tarehe 18 november mwaka huu wanakijij watano walipigwa hadi kulazwa hospitali walituchomea nyumba zetu moto na kibaya zaidi walimlazimisha kija aitwaye isanya Nabana kula gamba la nyoka"alisema Melau

Melau alisema kuwa wao kama wananchi wamekubaliana na mpango ulioanzishwa na tanapa wa ujirani mwema lakini kufuatia tabia ambayo tanapa wanaifanya ya kuwanyanya maeneo yao hawatakubaliana nayo kwani sheria hii walioanza na tabia hii inakinzana na maana nzima ya ujirani mwema.

'' Nauliza kuwa ni jirani gani mwema ambaye anachoma moto nyumba ya jirani zake na kuhamisha mipaka pamoja na kuvurga amani katika jamii"alisema Melau.

Kwa upande wake mjumbe wa serekali ya kijiji kimotorok Naishiye Ngoriayi naye alisema kuwa wao kama wanawake wamekuwa wananyanyaswa sana katika kijiji hicho kwani hata wakienda porini kutafuta kuni wamekuwa wanakamatwa na wamekuwa wakikamatwa wanalazimika kulipa shilingi 30000 kwa kila mmoja au wakati mungine ngombe wanakamatwa na wanachajiwa ela nyingi.

Alibainisha katika eneo hilo ambalo wanafukuzwa ndipo ambapo wanategemea watoto wao wakapate elimu maeneo hayo sasa wakiondoka wataenda wapi kupatiwa elimu kweli tunamuomba rais wetu atusaidie sana katika swala hili kwani tunateseka wananchi wake.

Akijibu  tuhuma hizo Kaimu mkurugenzi  muhifadhi mtokonologia ,idara ya Ikologia Jastini Muhando alisema kuwa eneo hilo lilikuwa la wazi kwani watu walitolewa mda mrefu  na lilikuwa kama pori la akiba ndipo watu hao wakaamua na wao kama tanapa hawawezi kuvamia maeneo bila ya kufata sheria.

Alibainisha kuwa wao hao sio wajinga kiasi kwamba wavamie tu maeneo ya watu bila kufuata sheria na walifuata sheria kwa kuwatafuta utaratibu wa ngazi zote za serekali kuanzia wilaya hadi kufikia katika ngazi ya mkoa na sio hao tu wakati wakifanya yote hayo walikuwa wanashirikiana na wananchi wenyewe hivyo hawakuweza kutumia nguvu ya aina yoyote kama wanakijiji hao wanavyosema .

“tuliona tufanye marekebisho ya mipaka hiyo na wanakijiji waliambiwa walete mapendekezo ili yaweze kwenda kwa mkuu wa mkoa na kibaya zaidi badala wanakijiji hawa kupeleka mapendekezo kwa mkuu wa mkoa ili wapate suluisho wakapuuzia nao wakapeleka malalamiko yao kwa waziri mkuuna kwa kweli siwezi sema uko kwa waziri waliambiwa nini”alisema Muhando.

Alisema kuwa  wao kama Tanapa pamoja na hayo hawakuona tatizo bali waliendelea kuuomba mkoa uwaite wanakijiji hao  ili waweze kuelezea mapendekezo ambayo mkoa wataalamu wameyapendekeza na kuyaona yanafaa lakini cha ajabu wanakijiji hawajasema chochote.

“alisema kuwa kwakuwa eneo hilo lilikuwa halina mwenyewe basi walikubaliana asiwe mwanakijiji wala tanapa wanavamia eneo hilo lakini wanakijiji hao hawakusikia  kwani eneo hilo ni la mgogoro  hivyo wanakijiji hawaruhusiwi kufeka maeneo haya kuongeza mashamba wala kuleta mifugo yao katika eneo hilo maana eneo hilo ni la mgogoro na haliruhusiwi kutumika na mtu yeyote awe tanapa wala mwanakijijina kwakweli wanakijiji hao hawakusikia na ninashaa upande wa kusini mwa orkapusai kuna eneo kubwa sana ambalo alina makazi na nieneo kubwa sana sasa wao hawataki kwenda uko wanakuja ktika eneo hilo na sababu kubwa ya kuja katika eneo hilo haionekani kwani haina hata maji  na nieneo ambaolo na kwakweli tukasema kuwa eneo kama halina eneo mtu mmoja awezi sema anaendeleza eneo hilo maana linamgomgoro hivyo tukasema wasifungue mashamba wala wasipeleke ngombe zaidi ya eneo ambalo wanalitumia”alisema Muhando.

Alibainisha kwa upande wa kusema wamechoma nyumba zao ni uongo kwani wananchi hawa pia walivamia eneo la watu ambalo zamani kulikuwa kunakaa na watu ambao wanatumia eneo hilo na waliaacha mahema yao baada ya  kuambiea wahame na walihama na kuelekea katika maeneo mbalimbali ikiemo kondo hivyo wanakijiji hao walipoenda wakavamia mahema yale na ndipo wao kama tanapa wakaamua kwenda na kuyabomoa mahema yale na yaliyofaa kuchomwa yalichomwa na waliwaamurisha watu hao warudishe vitu vyao katika katika eneo la mgogoro.

Muhando alisema  wakati wamekaa wanasubiri sasa hitimisho la mkuu wa mkoa ndipo wakasikia wanakijiji hawa wamewaita waandishi na kuzungumzia mgogo ro huo na wakati kabla ya kuwaita mkuu wa mkoa aliwauliza kuwa kwanini wanakijiji hawa wasifuate sheria kuanzia ngazi kwa ngazi wanini wameruka mkuu wa wilaya na kwenda kwa waziri moja kwa moja na aliwaamuru kuwa warudikwa mkuu wa wilaya ili wayazungumze na watuatu na ikishindikana kwa mkuu wa wilaya ndo waende katika ngazi zingine.

Alibanisha kuwa wao kama tanapa walikuwa wanasubiri mkuu wa mkoa wawakutanishe na wao kama tanapa hawawezi kuvamia na ndio maana waliwaita wapimaji ili wakapime na waliwatumia wale kwa vile waliamini kuwa kutokana na tangozo la serekali lilivyosema ndio maana waliwaita kwani wao wenyewe hawawezi kupima maana sio kazi yao kupima maeneo hayo ndo maana kuna wataalamu.

“sisi kama tanapa tunasema kuwa hatujatumia nguvu yoyote kuvamia kujiji chochot e na wao ndio wamevamia kwani tangu hifadhi hii ilivyoanzishwa mwaka 1970 hawakuwepo nabila shaka nathani hawa watu labda wamekuja 1980 na wametukuta ivyo wangefuata tu taratibu ukimkuta mtu katika eneo unamuuliza na unafata utaratibu wa kupim na kwa upande wa swala la kija kulazimishwa kula gamba la nyoka kwakweli hilo sio la kweli”alisema Muhando.

Aliwasihi wananchi hao kufuata sheria na iliyotolewa na watumie wataalamu kupima mipaka yake  na mgogo huo sio mkubwa sana mpaka ukuzwe kwani wanaweza kukaa chini na kurekebisha.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates