msaniii wa muziki wa kizazi kipya (bongo Flava) Abeli MOtika alimaarufu kwa jina la Mr .Ebbo mwenye umri wa miaka 37 amefariki dunia mkoani hapa.
Msani huyo amefariki dunia juzi saa nne usiku katika hospitali ya dream seminari inayomilikiw ana kanisa katoliki lililopo Usa river Wilalyani Arumeru mkoani hapa.
Akizungumza na Libeneke Nyumbani kwa baba wa marehemu kaka wa msanii huyo Olais Loshila Motika alisema kuwa marehemu Mr.Ebbo alifariki dunia jana usiku kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya damu.
Alisema kuwa marehemu alisumbuliwa na ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi tisa ambapo kabla ya kuumwa alikuwa anaishi mkoani Tanga na alipozidiwa aliletwa mkoani hapa kwa ajili ya matibabu na aliwahi kutibiwa katika hospitali nyingi ikiwemo Mounti meru ,KCMC pamoja na hospitali ya kanisa ya seliani.
Aidha alibainisha kuwa marehemu Mr.Ebbo ameacha mjane na watoto watatu na anatarajiwa kuzikwa December tano katika makaburi ya nyumbani kwao Masai Camp Olorieni ndani ya manispaa ya mkoa wa Arusha.
Loshika alisema kuwa wamepokea msimba huu kwa masikitiko makubwa sana kwani marehemu alikuwa anategemewa na familia hiyo pamoja alijuwa ni kioo cha jamii hivyo familia hiyo imepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Libeneke hili lilizungumza na mmoja wa washabiki wa msanii huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Ally Abdi alisema kuwa amepokea msiba huo kwa masikitikio makubwa sana kwani alikuwa anampenda msanii huyo sana na alisema kuwa anafurahishwa na kibao acha boda boda ambacho msanii huyo alikiimba kabla ya kuanza kuumwa.