SUGU AAHIDI KUKAMUA VILIVYO KWENYE ONYESHO LA ANTI VIRUS ARUSHA DECEMBER 18

 Wakwanza katikakati ni mbunge wa Mbeya mjini (Mr,Sugu) kulia kwake ni msanii Danny Msimamo na kushoto kwake ni mmoja wa kundi la mapacha (wajanja sapplayaz) wakiwa wanaongea na waandishi wa habari kuhusiana na Tamasha hilo la Anti virus
Sugu akiwa anaongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Triple A
Wasanii mbalimbali wakiongonzwa na mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Josephy Mbilinyi wanatarajia kufanya Tamasha lijulikanalo kwa jina la   Anti virus mapema december 18 mwaka huu katika uwanja wa ukumbi wa TripleA uliopo jijini hapa .

Akiongea na waandishi wa habari msemaji Josephy Mbilinyi alisema kuwa Tamasha hilo linaambatana na uzinduzi wa albamu ya Anti virus ambayo itawashirikisha wasanii mbalimbali wa kizazi kipya  wa  mjini hapa pamoja na wasanii wa mbalimbali .

Alisema kuwa nia ya tamasha hilo ni kutangaza matatizo ya wasanii kwani wamelalamika kupitia nyimbo zao lakini wameona haifai ndo maana wakaamua kutangaza matatizo haya kupitia tamasha hilo.

Alisema wanampango wa kutangaza tamasha hilo nchi nzima ili kuweza kuwapa wa moyo wasanii ambao wapo mikoani lakini bado hawajaweza kusikika.


Alibainisha kuwa anti virus ni  muungano  wa wasanii ambao wameamua kupambana kwa  ajili ya kuwakomboa wasanii wenzao ambao wana vipaji lakini wameshindwa kujiinua pia kundi  hili linajihusisha na kurekodi albamu ambazo zinaelezea matatizo ambayo wasanii wanayo na wanakaa na kuweza kujadili nini kifanyike ili waweze kukomboa maisha ya wasanii.

"wote tunajua kuwa katika sekta za ambazo zimetelekezwa ni hii ya wasanii hivyo tamasha hili linajitaidi kufanya hivi ili kutafutawatu wa kuwasaidia kwa kupitia vitu hivyo ikiwa ni wanarekodi na pia tunachukuwa wasanii wa kiwango cha chini  "Alisema mbilinyi

Alibainisha kuwa katika tamasha hilo wanahaidi kuwa watafanya kitu ambacho akijawahi kufanyika katika mji wa Arusha na itakuwa ni mara ya kwanzakufanyika.

Aliwataja baadhi ya wasanii ambao watakuwepo ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye anaongoza kundi hili la Ant Virus Sugu  wengine wakiwa ni MKoloni,Rama dee,Suma G, Coin,Isaya Family, peen Lawyer ,Danny Msimamo pamoja na Mapacha wajanja sapplaya.

Alisema kuwa pia kutakuwa na wasanii wengine ambao hawajashiriki katika albamu hiyo ya Anti virus ambao aliwataja kuwa ni Sister P,mabaga fresh na pia alisema kuwa kwa upande wawasanii wadogo wametoa nafasi kwa wasanii wa hapa hapa mkani Arusha ambapo alisema kuwa watakuwepo Mo kweli ,jambo  Squid,,pamoja  na Bu nokos .

"unajua asilimia tisini na tisa pointi tisa wanatutia moyo na wanatusaidi ila si unajua watu wote hawawezi kuwa manesi ndo maanakuna walimu nanathani jinsi tunavyoenda wataongezeka bwana"alisema Sugu

Alimalizia kuwa tamasha hili ni maalumu kwa ajili ya kupigania wasanii warudi kazini wasikae mitaani tu bila kazi na wajitaidi kufanya kazi maana ukombozi upo.

Alisema kuwa Tamasha hili ni endelevu kwakuwa ni tamasha la mkusanyiko wa wasaniii tofauti tofauti na tamasha hili sio biashara bali mi maendeleo na litaendelea hadi mwisho.

Alitoa wito watu wa Arusha kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tamasha hili  ili wasanii wao waone kuwa wamejitokeza kuwainua alibainisha kuwatiketi zitauzwa kuanzia saa sita mchana na shoo itaanza saa kumi jioni hadi saa sita usiku huku kiingilio kikiwa 5000 na katika masaa hayo kutakuwa nasektioni mbili ambapo wasanii wataimba  moja kwamoja kwa mdundo huku lisaa limoja likitumika kwa ajili kuzindua albamu hiyo ya anti virus.

Alisema kuwa hali ya usalama iko vizuri kabisa kwani wanajaribu kuwaaminisha watu kuwa wanaweza pasipo shida

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post