Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI WA AICC WAPATA MAFUNZO YA UKIMWI

TAASISI na mashirika mbalimbali ya umma nchini, yametakiwa kujiwekea utaratibu wa kutoa elimu ya ukimwi kwa wafanyakazi wao sanjari na kulinda haki za waathirika ikiwemo kutowanyanyapaa ,hatua ambayo itasaidia kupunguza kasi yamaambukizi mapya ya ukimwi.    

Rai hiyo imetolewa na mwendeshaji wa semina dkt.Julius Onesmo kwa wafanyakazi wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha(AICC)inayotolewa kila mwaka, ikilenga kutoa elimu juu ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na kupima kwa hiyari kwa wafanyakazi wa kituo hicho.

Alisema kuwa ipo haja kwa taasisi na mashirika ya umma nchini kujiwekea utaratibu kama huo wa kutoa elimu juu ya maambuziki mapya ya virusi vya ukimwi(VVU)ambayo imeolekana kuwa na mafanikio kwa wafanyakazi hao.

Alisema hatua hiyo itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza kasi ya maambukizi  ya VVU hususani mahala pa kazi na kwenye mikusanyiko , kwa mujibu wa Onesmo takwimu zinaonyesha kwamba  maambukizi hayo yameshuka kutoka asilimia 7 ya miaka ya nyuma  hadi kufikia asilimia  5 mwaka huu hapa nchini.

Aidha alisema jamii imekuwa ikiwanyanyapaa watu wenye maambukizi ya VVU na ukimwi, sehemu zenye mikusanyiko ikiwemo mahala pa kazi, hali ambayo huwafanya wajisikie wametengwa na jamii na kusababisha wengi wao kuathirika kisaikolojia na wengine kupoteza maisha kabla ya muda .

‘’jamii imekuwa ikiwachukuliwa wenye VVU kama watu waovu wenye kukiuka maadili ya jamii na dini na kuwanyanyapaa ,hali hiyo haita komesha maambukizi nchini ni lazima tuwajali na kuwapenda waathirika’’alisema.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa AICC Elishilia kaaya alisema kuwa semina kama hizo wamekuwa wakizifanya kila mwaka kwa wafanyakazi lengo ni kuwakumbusha hali halisi ya maambukizi ya ukimwi na kupima kwa hiyari.

Alisema iwapo kila taasisi nchini zitaungana nasi walau mara moja kila mwaka kutenge siku moja tu ya kutoa semina kwa watumishi juu ya maambukizi ya VVU na kupima kwa hiyari,kutasaidia sana kuepusha na kupunguza maambukizi mapya ya VVU.

‘’sisi hapa AICC tumejiwekea utaratibu kila mwisho wa mwaka hususani siku ya ukimwi duniani inayofanyika kila mwaka desema moja,tunaandaa semina kwa wafanyakazi wetu kukumbushwa na kupima kwa hiyari kuangalia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi’’alisema

Hata hivyo aliwasihi wafanyakazi wenye kujitambua wanaishi na virusi vya ukimwi kutokuwa waoga kujitangaza kwani sera ya nchi kwa mujibu wa ibara ya 12(1) ya katiba inakataza mtu ama kikundi kumnyanyapaa mwathirika wa ukimwi.

Post a Comment

0 Comments