CHAMA cha
riadha mkoani Arusha(ARAA) kimeingia katika kashfa nzito baada ya mwenyekiti
wake,Henry Nyiti kudaiwa “kuchakachua”katiba ya chama hicho hali ambayo imezua
mgogoro mzito ndani ya chama hicho.
Baadhi ya
wajumbe na viongozi wa chama hicho wamemtuhumu mwenyekiti wao,Nyiti kuwa
ameshiriki kupitisha katiba batili kwa lengo la maslahi yake binafsi.
Wakizungumza
na libeneke hivi karibuni kwa nyakati tofauti bila kutaja majina yao hadharani
walimtuhumu Nyiti kwamba amepitisha katiba ambayo haina Baraka kutoka kwao .
Walisema
kuwa katiba iliyopo kwa sasa ni batili kwa kuwa haijapitishwa na mkutano mkuu
wa chama hicho .
“Katiba ya
sasa ni batili kabisa kwa kuwa sisi kama viongozi hatujaipa Baraka na wala
haikupitishwa na mkutano mkuu wowote na mwneyekiti wetu ana maslahi yake
binafsi ndani yake”walisema kwa nyakati tofauti
Akijibu
malalamiko hayo kwa njia ya simu jana,Nyiti alikanusha vikali na kudai kuwa
hayo ni majungu yasiyo na tija huku akisisitiza kuwa katiba iliyopo kwa sasa
awali ilikuwa na mapungufu madogo madogo lakini amejitahidi kuyatatua.
Aliyataja
baadhi ya mapungufu hayo ni pamoja na katiba hiyo kutogongwa muhuri wa na idara
ya usajili wa vyama vya michezo nchini
lakini tayari suala hilo liimeshatatuliwa.