Mkuu wa wilaya ya
Kasulu mkoani Kigoma,Dan Makanga kwa kushirikiana na baadhi ya askari wa kitengo
cha upelelezi cha jeshi la polisi mkoani Arusha wamedaiwa kuingia na kisha kupekua nyumba
na ofisi ya mfanyabiashara wa utalii jijini Arusha,Mathew
Mollel wakipekua hati ya kiwanja aliyodai kutapeliwa kiongozi huyo.
Tukio
hilo lililovuta hisia za watu wengi jijini hapa hivi karibuni jijini
Arusha limedai kwamba mkuu huyo wa wilaya aliongozana na askari hao
wawili hadi katika ofisi ya mfanyabiashara huyo
iliyopo jengo la hoteli ya New Safari ambapo mbali na upekuzi huo
alidaiwa
kuwamuru wavunje safe ya mfanyabiashara huyo kwa lengo la kupekua hati
ya
kiwanja.
Tayari jeshi la
polisi kupitia kwa mkuu wa upelelezi mkoani Arusha,(RCO) Duwani Nyanda limekiri
kutokea kwa tukio hilo ambapo juzi wakati akihojiwa na gazeti hili alisema kuwa
ni kweli askari hao walitumwa kupekua nyumba na ofisi hizo kwa kuwa mfanyabiashara huyo anakabiliwa na kesi
ya kughushi na kisha kujipatia mali kwa
njia ya udanganyifu.
“Ni kweli nilituma
vijana wangu na huyo mtu ana kesi ya kughushi na kujipatia mali kwa njia ya
udanganyifu “alisema Nyanda
Haahivyo,alipoulizwa
kuhusu madai ya Makanga kuwaamuru askari wake kuvunja safe ya mtuhumiwa huyo
Nyanda alikwepa kuzungumzia suala hilo lakini alijibu kwa kifupi”Kwani kuna
ubaya akiwepo? alikuwa ana identify(anahakiki) mali zake zilizoibiwa”.
Akihojiwa na gazeti
hili,Mollel ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Raimbow Tours and Shuttle
alidai kuwa mnamo Agosti 21 mwaka huu askari wawili waliwasili katika ofisi
yake na kumtaka kufika katika ofisi ya mkuu wa idara ya upelelezi mkoani Arusha
kwa madai anakabiliwa mashtaka mbalimbali.
Mollel,kwa huzuni
alidai kuwa aliitikia wito huo na kisha ambapo aliwasili katika ofisi hiyo na
kisha kumkuta Makanga akiwa na baadhi ya askari ambapo alisimulia kwamba alinyang”anywa
simu zake mbili za mkononi na askari hao ambapo walimtaka kutowasiliana mtu
yoyote.
Hatahivyo,alisema
kuwa mnamo Agosti 22 mwaka huu aliwasili
tena katika ofisi hiyo na kisha kuamriwa kuelekea katika ofisi yake ambapo waliongozana
na askari hao wawili,Makanga pamoja na mtu mmoja aliyemtambua kwa jina moja la
Shija ambapo mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo walianza kufanya upekuzi
wa hati hiyo.
“Baada ya kupekua
kila sehemu mheshimiwa mkuu wa wilaya aliwaambia askari wavunje safe ili
kuipekua hati hiyo lakini niliwaambia funguzo ziko nyumbani ndipo tukaongozana
hadi Mianzini nyumbani kwangu wakaanza kupekua hadi chumbani”alisimulia Mollel
Mollel,alidai kuwa
mara baada ya kufanikiwa kuchukua nyaraka hizo ndipo alipofanikiwa kuwasiliana
na wakili wake aliyemtaja kwa jina la Duncan Ooola na walifika tena katika
ofisi ya upelelezi mkoa ambapo alikabidhi hati hiyo ambayo hadi sasa
inashikiliwa na ofisi hiyo na kudai ameamriwa kuripoti kila jumatano ya wiki.
Kwa mujibu wa maelezo
ya Mollel alisimulia kuwa chanzo cha mgogoro huo ni kwamba mamo 1997 Makanga
alimpatia kiwanja hicho kwa makubaliano ya kujenga nyumba ya kuishi na familia
yake ambapo na pindi atakafanikiwa kupata sehemu nyingine atalazimika kukiachia
kiwanja hicho lakini mwaka 2007 alimua
kutafuta hati ya kiwanja hicho kwa kuhofia eneo hilo kumegwa na wakala wa
barabara nchini(Tanroads) mkoani Arusha.
Kwa upande wake mkuu
wa wilaya ya Kasulu(Makanga) alipohojiwa kwa njia ya simu juzi alikiri kuwa
jijini Arusha tarehe ya tukio na kudai
alishiriki hatua kwa hatua kwa kuwa alikuwa anahakiki mali zake alizodai
kutapeliwa na mfanyabiashara huyo.
Hatahivyo,Makanga
alikanusha vikali madai ya kuwaamuru askari hao wavunje safe la mtuhumiwa huyo
huku akisisitiza kuwa alifanikiwa kuipata hati hiyo ambayo hatahivyo alidai
ilibadilishwa jina kiujanja.
“Ni kweli nilikuwa
Arusha hii ni kesi kubwa nilikuwepo kwenye tukio ili kushuhudia mali zangu
lakini sikuamuru ivunjwe safe kwani
tulifanikiwa kuipata hiyo hati”alisema Makanga
Tukio hilo linatajwa
kuzivuruga familia mbili za Mollel na Makanga huku ikielezwa ya kwamba watu hao
wameoa katika familia moja wilayani
Bariadi mkoani Shinyanga
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia