Ticker

6/recent/ticker-posts

HUDUMA MPYA YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAZINDULIWA NA LAPF KWA WANACHAMA WAKE

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akitoa neno kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu‘Piga Kitabu na LAPF’
Uzinduzi rasmi wa Piga Kitabu na LAPF ulipambwa na shamrashamra za aina yake.
Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Hawa  Ghasia, akimkabidhi mfano wa hundi Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,  Rolland Lyamuya mkopo wa elimu ya juu kupitia huduma mpya ya mikopo kwa wanachama wa mfuko huo iitwayo ‘Piga Kitabu na LAPF’  iliyozinduliwa juzi jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa Piga Kitabu na LAPF Mh. Hawa A. Ghasia akipokea zawadi ya kitabu cha Nelson Mandela kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa  Pensheni wa LAPF.
 Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ Mkopo wa elimu ya juu kwa wanachama wa LAPF iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Vijana kutoka Kigamboni Community Centre wakitoa burudani ya ngoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ huduma mpya ya mikopo ya eilimu ya juu kwa wanachama wa LAPF, iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.

Post a Comment

0 Comments