Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma Nkamia akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi wa Nembo ya radio Triple A fm na kuwataka wamiliki na wanahabari kuhakikisha wanafuata maadili ya taaluma ya uandishi wa habari iwe kazini au nje ya kazi zao.
Serikali
imesisitiza kuwa haitavifumbia macho vyombo vya habari vitakavyo kiuka
maadili ya habari na kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali vyombo
hivyo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari vijana utamaduni na michezo
Juma Nkamia wakati akizindua logo ya redio Triple A fm jijini hapa huku
akiwataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao iliwaweze kuitumikia
jamii
bila ya kuleta uchochezi kwa jamii utakaopelekea uvunjifu wa amani.
Naibu Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia akiwa na Bodi ta wakurugenzi wa Kampuni ya The Blue Triple A Ltd ambayo ni kampuni tanzu ya Radio Triple A fM inayoongozwa na Mkurugenzi wake kulia na kushoto Mr&Mrs Papa King Mollel wakiwa katika picha ya pamoja baada ya naibu waziri kuzindua nembo ya Radio hiyo jijini hapa
Nkamia
alisema kuwa Taaluma hiyo inaweza kuileta jamii katika kukabiliana na
mmomonyoko wa maadili uaoendelea hapa nchi au kuzidi kuumomonyoa maadili
hayo kwani wao kazi yao ni kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha jamii
inayovizunguka vyombo hivyo hivyo vinamchango mkubwa katika maendeleo ya
taifa.
"Lengo
hapa ni kuhakikisha kuwa vymbo vya habari haviwi ndio kichocheo cha
uvunjifu wa amani ila nawasihi muwe kichocheo katika suala zima la
kupiga vita mmomonyoko wa maadili yetu kwa nyinyi mpo karibu zaidi na
jamii"alisisitiza Nkamia
Kwa
Upande wake Meneja wa Tcra kanda ya kaskazini Anethy Matindi aliwakemea
mablogger kwa kupachika picha zinazo vunja sheria za nchi ikiwemo pia
kupachika picha
zisizofaa kwa jamii na kuwa dawa yao ipo inakuja
Baadhi ya viongozi wa serekali wa jiji la Arusha nao waliudhuria uzinduzi huo
Matindi
alisema kuwa imekuwa ni tabia kwa vyombo vya habari kutofuata maadili
hivyo akavitaka kuacha mara moja kutumia vyombo hivyo kwa kukiuka
taaluma na weledi wa tasnia hiyo
Naye
meya wa jiji la Arusha Gaudency Lyimo alisema kuwa anaipongeza Triple A
Fm kwa kuweza kusogeza habari kwa jamii ya wakazi wa jiji la Arusha
ambapo taarifa zimekuwa zikifika kwa wakti hivyo kuchangia kukua kwa
sekta mbali mbali na kuleta maendeleo kwa jamii
Meya wa Jiji la Arusha Gaudensi Lyimo akitoa nasaha chache kwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa blue Frem uliopo kwenye klabu ya usiku ya TRIPLE A NIGHTY CLUB ya jijini hapa
Mkurugenzi
wa The Blue Triple A Ltd Papaa King aliwashukuru viongozi wote
waliohudhuria katika uzinduzi huo huku akitabaisha kuwa Redio hiyo
itafuata taratibu zote za kisheria katika kujiendesha ikiwemo kuwapa
maslahi mazuri wafanyakazi wake iendane na viwango
.
Sehemu ya wafanyakazi wa Radio Triple A fm wakiwa katika picha ya pamoja
kulia na kushoto kwa naibu waziri Nkamia ni Meneja wa redio hiyo Fredy Mumburi kushoto ni mkurugenzi wa redio hiyo Papa king molel baada ya uzinduzi wa
logo ya redio hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki picha kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog
Tags
matukio burudani