TASWIRA YA TAMASHA LA FIESTA 2014 LILIVYOSAMBAZA UPENDO WAKUTOSHA KWA WAKAZI WA MUSOMA


Wasaniii walioshiriki tamasha la Fiesta 2014 wakiwa na mishumaa jukwaani wakisambaza upendo na kuwafariji wale wote waliopotelewa na ndugu zao,waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea  hivi karibuni wilayani Butiama mkoani Mara,ambapo watu zaidi ya 40 walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa musoma wakiwa ndani ya uwanja wa Karume,wakati tamasha la Fiesta 2014,likiendelea huku shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala kila kona ya uwanja.
 Madansa wa msanii Rachael wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani
 Msanii Rachael akiimba kwa hisia jukwaani kwenye tamasha la Fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Karume,mjini Musoma.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Barnaba ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la Waharade akiwaimbisha wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la fiesta 2014
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Barnaba ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la Waharade akiwaimbisha wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la fiesta 2014
 Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Weusi ,Nick wa Pili akiwarusha wakazi wa mji wa Musoma usiku huu kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika ndani ya uwanja wa Karume.
 Sehemu ya wakazi wa Musoma waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume
 Nick wa Pili akikamua jukwaaani
 Shilole akiimba kwa hisia jukwaani.
  Mwanadada machachari awapo jukwaani,Shilole akiimba kwa madaha kabisa kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Mmoja wa wanamuziki mahiri ,Christian Bella ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa nani kama Mama,akiwaimbisha wakazi wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta usiku huu.
 Pichani kati ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael akiwa sambamba na madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta vilivyo usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma
 Mashabiki wakishangilia burudani iliyokuwa ikitolewa na wasanii mbalimbali jukwaani usiku huu
 Mmoja wa wasanii anaeokuja juu katika anga ya muziki wa hip hop,Young Killer a.k.a Msodoki akiimba jukwaani.
 Ulifika wakati wa kutoa pale na kusambaza upendo kwa wakazi wa Mji wa Musoma na Vitongoji vyake,kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso na kupoteza maisha ya zaidi 40.
  Mmoja wa wasanii anaekuja juu katika anga ya muziki wa hip hop,Young Killer a.k.a Msodoki akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Kaume.
 Wakazi wa Musoma walivyojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014 katika uwanja wa Karume usiku huu.
 Jicho la samaki  likiwa limewakusanya pamoja mashabiki wa tamasha la Fiesta lililokuwa likiendelea ndani ya uwanja wa Karume,mjini Musoma.
 Wakali wa hip hop,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kwa wimbo wao uitwao huko kwenu vipi,huku miluzi na shangwe za mashabiki zikiwa zimetawala uwanjani hapo.

Msanii wa hip hop katika miondoko ya Bongofleva atambulikae kwa jina la kisanii Roma,akitumbuiza jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa mjini Musoma kwenye tamasha la fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Karume.
Wasanii wa Kundi la Wanaume TMK,a.k.a Wakata Mkaa Themba na Chege wakilishambulia jukwaa la fiesta lililofanyika katika uwanja wa Karume,mjini Musoma ambao maelfu ya watu walijitokeza kulishuhudia tamasha hilo.


About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.