WASHINDI WA TUZO ZA HABARI ZA TANAPA WATEMBELEA KIJIJI CHA UTALII WA UTAMADUNI AFRIKA KUSINI CHA LESEDI
Posted by
woinde
on
Thursday, September 18, 2014
in
Habari
utalii
|
|
Mshindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 Gerald Kitabu (The Guardian) akisalimiana na
kijana wa Kizulu katika kijiji cha Utamaduni cha Lesedi walipotembelea ili
kujifunza utalii wa kiutamaduni nchini Afrika Kusini.
|
|
Mshindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 Vedasto Msungu (ITV) akisalimiana na kijana wa
Kizulu katika kijiji cha Utamaduni cha Lesedi walipotembelea ili kujifunza
utalii wa kiutamaduni nchini Afrika Kusini.
|
|
Katika
Utamaduni wa Kizulu boma hulindwa na mlinzi anayekaa juu kwa ajili ya kuangalia
waingia na watokao kama anavyoshuhudiwa hapa alipotembelewa na Washindi wa Tuzo
za Habari za TANAPA 2013 nchini Afrika Kusini.
|
|
Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 kutoka kulia Gerald Kitabu, David Rwenyagira
na Vedasto Msungu wakifurahi pamoja na wanakijiji cha Wazulu cha Lesedi
walipowatembelea ili kujifunza utamaduni |
|
Mshindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 David Rwenyagira (Radio Five) akishika ngao
kwa ajili ya kujikinga na adui ambao ni mojawapo ya utamaduni wa Wazulu.
|
|
Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiendelea kupata somo juu ya tamaduni
mbalimbali zinaopatikana nchini Afrika
Kusini.
|
|
Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 katika picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa Kituo cha Utamaduni cha Lesedi, Afrika Kusini.
|
|
Lugha
ya Kiswahili nayo yafahamika vema Afrika Kusini kama inavyoonekana hapa katika
picha iliyopigwa na Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013.
|
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia