Afisa ufundi wa kilimo cha mboga
kutoka TAHA Bw. Abdon akiwaelekeza wakulima kuhusu mbinu bora za
uoteshaji wa miche ya mboga kwenye trei maalumu katika mahadhimisho ya
siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame
katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Bi.
Zuhura Chikira ambaye alikuwa mgeni rasmi, akisiliza maelezo kutoka kwa
mtaalamu wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Giliard Daniel katika
mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha
Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Shamba mfano namba 1
Shamba mfano namba 2
Shamba mfano lililotumika kuwafundishia wakulima siku hiyo
Mzee Shabani Shoo akizungumza na wakulima (hawapo pichani)kuhusu mbinu alizofundishwa na wataalamu
wa TAHA na kuweza ukuaji bora wa zao lake la kabeji ikiwa ni pamoja na ongezeko la idadi ya mazaokutoka kabeji 4000-18000
Wakulima wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya mbolea na viatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi.Baby Nkassa
wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viatilifu kwenye mazao
Wakulima wa Kijiji cha
Silversand-Machame wakifuatilia mafunzo ya namna bora ya uandaaji wa
udongo kwa ajili ya kuotesha miche ya mbogamboga
Wakulima waliohudhuria mafunzo ya kilimo cha mboga katika siku ya wakulima shambani wakifuatilia hotuba kutoka kwa mgeni rasmi
Wakulima wakifatilia maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga mboga kutoka TAHA Bw.Collins Okiyawakati wa mafunzo hayo
Asasi
ya sekta binafsi ya wakulima wa mboga mboga,Matunda, maua, viungo na
mbegu zake imehadhimisha siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa
kijiji cha Mferejini-Machame katika wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Maadhimisho
hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya Mwezi mmoja mpaka miwili ili
kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za kilimo cha mazao ya
‘horticulture’ ikiwa ni sambamba na kujifunza mbinu fasaha za kilimo
biashara.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia