Ticker

6/recent/ticker-posts

MWANARIADHA MLEMAVU OSCA PASTORIOUS HATIANI


Mwanariadha mlemavu wa Afrika
Kusini Oscar Pistorius, amepatikana
na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva
Steenkamp pasi na kukusudia.

Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile
Masipa alisema kuwa mwanariadha
huyo alimuua Reeva kwa bahati
mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa
mlango wake wa choo akiwa akatika
hali ya mshtuko akidhani kuwa
jambazi alikuwa amevamia nyumba
yake.

Alisema kuwa upande wa mashitaka
umeshindwa kuthibitisha kuwa
Pistorius alinuia kumuua Steenkamp
na kwamba alifanya mauaji hayo kwa
kusudi.

Pia alipatikana na hatia ya kosa la
kutumia silaha yake visivyo
alipokwenda mgahawani.

Jaji Thokozile Masipa amesogeza
muda wa mwanaridha huyo yuko
huru kwa dhamana.
Pistorius atakuwa huru hadi hukumu
itakapotolewa mwezi ujao, ambapo
anaweza kuhukumiwa hadi miaka 15
gerezani.

Oscar Pistorius ataendelea
kukaa kwa mjombake alikokuwa
muda wote kesi ilipokuwa
ikiendelea.

Mjombake Pistorius, Arnold Pistorius
amemshukuru Jaji Masipa kwa
uamuzi wake wa kumuachia kwa
dhamana.

Post a Comment

0 Comments