Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA SIMU YA AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU IKWA SHULE ZA SEKONDARI ZA DAR

 Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Sekondari Manispaa ya Temeke, Yasintha Kayoza kwa niaba ya shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario.
  Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), akiangalia moja ya vitabu vya masomo ya sayansi baada ya kuvikabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4.5/-,  kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana.
 Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 1.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana. Sekondari nyingine zilizokabidhiwa vitabu hivyo ni pamoja na Mvuti na Kambangwa. Kushoto ni Mwakilishi wa Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwalimu Sueiba
Mfinanga.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Shule Yetu’ kukabidhi vitabu hivyo vyenye thamani ya milioni 4.5/- kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.

==========  ========  ========
Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Dar
·         Zaidi ya shule 30 kufaidika na msaada wa vitabu kwa mwaka
huu,  kupitia mradi wa Airtel “Shule yetu”

Dar es Salaam, Jumanne 9 septamba 2014, Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel kupitia mpango wake wa “shule yetu” umeendelea na mpango wake
wa kuchangia katika kusaidia sekta ya elimu nchini ambapo  leo imetoa
msaada wa vitabu kwa shule 3 za sekondari jijini Dar es saalam

Shule zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Kambagwa sekondari
iliyopo wilaya Kinondoni,  shule ya sekondari Mvuti iliyopo wilaya ya
Ilala na shule ya sekondari Mbagala iliyopo wilaya ya Temeke ambapo
kila shule imepata vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja na
laki tano.

Akiongea wakati wa kukabithi vitabu hivyo, Meneja huduma kwa jamii
Airtel Bi Hawa Bayumi alisema”  Tunayofuraha kuendelea na mpango huu
wa “shule yetu”  kwa mwaka huu na kuwa na shule mpya zitakazofaidika
na vitabu vya masomo ya Sayansi. Tunazo shule zaidi ya 30 ambazo
tumezipata kwa kushirikiana na uongozi wa serikali zitakazofaidika na
msaada huu wa vitabu kwa mwaka huu,  Na leo tumeweza  kuzifikia shule
za Kambagwa, Mvuti na Mbagala na kuwapati  vitabu vitakavyoweza kuleta
tija katika ufaulu na elimu kwa ujumla”.

“Nia yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya
elimu katika kuinua sekta ya elimu nchini huku tukiwekea mkazo katika
masomo ya sayansi kwani tuaamini ulimwengu na nchi inahitaji
wanasayansi wengi ili kwenda na kasi ya ukuaji wa technologia. natoa
wito kwa walimu na wanafunzi basi watumie vitabu vizuri na kuweza
kuongeza wanafunzi wengi katika masomo ya sayansi na hatimae kuongeza
ufaulu zaidi.aliongeza” Bayumi

Akiongea kwa niaba ya walimu wakuu wa shule zilizopokea msaada jijini
Dar es saalam, Mwalimu mkuu wa shule ya Mbagala Bi Marcelina  Kimaro
alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa  kutufikia leo, tumekuwa
tukiona shule nyingi zikifaidiaka na mpango huu wa “Shule yetu” na leo
tunayofuraha kupokea msaada wa vitabu vya  Hisabati, Chemia, physikia
na Baiologia kutoka Airtel

Shule hii ya mbagala Sekondari ina jumla ya wanafunzi 2031 na uwiano
wa vitabu kwa wanafunzi kwa sasa ni kati ya kitabu kimoja kwa
wanafunzi wa 3 au 4 , kwa msaada huu leo utasaidia kupunguza
changamoto tuliyonayo ya uhaba wa vitabu na kufanya uwiano kuwa kitabu
kimoja kwa wanafunzi wawili. Halikadhalika msaada huu utatupatia
urahisi katika kusoma na walimu kuandaa masomo yao.

Kimaro aliongeza kwa kusema” Vitabu hivi vimetupa changamoto  kubwa ya
kuongeza juhudi katika masomo kwani nyenzo sasa tunazo na tunaamini
wanafunzi wetu wa masomo ya sayansi watasoma kirahisi na hatimaye
kupata  idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi.
Tunawaahidi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa faida ya wanafunzi
na jamii kwa ujumla”

Chini ya mpango wa “shule yetu” Airtel imeweza kutoa msaada wa vitabu
kwa shule za sekondari zaidi ya 1000 nchini huku mpango ukiwa ni
kizifikia shule nyingi zaidi kila mwaka

Post a Comment

0 Comments