Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
MATUKIO ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi
ya maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio hili kijana Gabriel
Mwasyebule miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu
kwa imani za kishirikina.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa
kifo hicho na kumtaja marehemu aliyetambulika kwa jina la Gabriel
Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande (Lwangwa) Wilaya
ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha
kali sehemu za kichwani na kifuani.
Alisema tukio hilo lilitokea siku ya jumapili majira ya saa tano asubuhi
huko katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya
Busokelo, Wilaya ya Rungwe, mkoaniMbeya
Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi wa kimila kijijini hapo
uliitisha kikao cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji
jirani na ndipo waliamua kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria
katika kikao hicho na kisha kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.
Alisema marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mshirikina kijijini hapo
kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao mengi ya mavuno ya
viazi na kujipatia pesa zilizowezesha ujenzi wa nyumba yake aliyoweka
marumaru na Gipsam pia kumiliki pikipiki moja huku akitarajia baada ya
mavuno mazuri ya mwaka huu kununua gari la kutembelea.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia