Ticker

6/recent/ticker-posts

JK AWATUNUKU WANAJESHI NISHANI YA MIAKA 50 YA JWTZ

 
Rais Jakaya Kikwete jana amewatunuku Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanajeshi 59.
Aidha Rais Kikwete pia aliwatunuku nishani ya Operesheni Safisha Msumbiji dhidi ya kikundi cha Lenamo mwaka 1986 hadi 1988.

Nishani hizo zilitolewa jana kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu, katika Chuo cha Mafunzo ya maafisa wa Jeshi Tanzania, kilichopo wilayani Monduli na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Mwinyi.

Katika Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya JWTZ, jumla ya maafisa 22 walitunukiwa nishani hizo huku ya Operesheni Safisha Msumbiji ilitolewa kwa makundi, ambapo maafisa waliopo kazini 14, waliostaafu 17 na waliofariki dunia sita.

Kwa upande wa maafisa walioshiriki operesheni hiyo ambayo wamefariki dunia waliwakilishwa na familia zao.

Awali Rais Kikwete, alishiriki maadhimisho ya hitimisho la zoezi la Medani zilizo ambatana na maonyesho mbalimbali ya kupambana na vita kwa njia ya anga na nchi kavu.

Kwenye maadhimisho hayo aliahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazikwa Jeshi hilo kwa kuwapatia dhana za kisasa ili waweze kupambana na matukio ya kiharamia na kigaidi yanayoibuka kwa kasi duniani.

Post a Comment

0 Comments