BREAKING NEWS

Friday, July 22, 2011

Dr. HOSEA ATOA KALI ADAI WATUHUMIWA KESI YA KAGODA WAMEKUFA

MKURUGENZI TAKUKURU Dk.Edward Hosea amevunja ukimya kuhusu suala la Kagoda kwa kudai kuwa ushahidi wa kesi Kagoda uligonga mwamba baada ya kuonyesha kuwa wadhamini na wakurugenzi wa kampuni hiyo wamekufa na picha zao kukutwa kwenye fail na kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa Kagoda Yusuf Maji aliwasilisha billion 40 ikiwa ni agizo

Mtuhumiwa anadaiwa kuwasilisha fedha hizo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa ikiwa watuhumiwa watajisalimisha na kurudisha fedha hizo watasamehewa

Dk.Hosea akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika Hotel ya Naura Spring ,Mkoa wa Arusha ,katika semina ya wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari alisema kuwa kesi hiyo ilikwamishwa na ushahidi wenye utata kwa kubainika kuwa ni marehemu na kuwa ni vugumu kumfanyia uchunguzi marehemu .

Mkurugenzi huyo alisema kwa kuwa kesi ya Kagoda imekuwa ni agenda kuu ya umma ,TAKUKURU inajipanga kurudia kufanya uchunguzi kuwa mafanikio ya kupata ukweli wa sakata hilo ,yatategemea ushahidi na kuomba watu wenye ushahidi wa sakata hilo wajitokeze kusaidia taasisi hiyo.

“Kwa maslahi ya umma na kutaka umma uridhike na sakata hili ,tutarudia uchunguzi kama TAKUKURU ,tofauti na awali tulivyotumwa na Rais kufuatilia Kagoda ,na ninataka niwahakikishie wananchi kuwa TAKUKURU ,tunajiendesha wenyewe na hutuendeshwi na Rais kama wengi wanavyodhani na sheria ya Rushwa inaeleza bayana .

Aidha alimtaka mwandishi wa habari aliyemtaja kwa jina la Mbaraka Ismahili aliyedai anaushahidi wa Kagoda aupeleke ili usaidie ushahidi .

Katika hatua nyingine Dk.Hosea ,amemsafisha Mbunge Andrew Chenge kuhusu tuhuma za Rada na kudai kuwa hausiki na tuhuma hizo ,kuwa Mbunge huyo anachunguzwa kuhusu tuhuma Vijisenti.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates