BREAKING NEWS

Thursday, July 28, 2011

RADIO 5 MABIGWA TAMASHA LA WAANDISHI

TIMU ya soka ya kituo cha Radio 5 juzi, imetwaa ubingwa wa soka katika tamasha la waandishi wa habari kanda ya kaskazini, baada ya kuichapa kwa penati 5-4 timu ya Pepsi ya Arusha.

Katika Tamasha hilo ambalo lilifanyika viwanja vya General Tyre kwa kushirikisha timu sita, Radio 5 ilifika fainali baada ya kuishinda kwa penati 10-9 timu ya TASWA toka jijini Dar es Salaam baada ya kutoka sale.

TASWA dar es Salaam, ndio walikuwa mabingwa watetezi wa soka kwa miaka miwili mfululizo katika bonanza hilo ambalo hufanyika kila mwaka kwa kuandaliwa na TASWA Arusha na kampuni ya Ms Unique promotion.

Pepsi ambayo ilialikwa katika michuano hiyo, pia ilifika fainali baada ya kuitoa kwa penati TASWA Arusha, 5-3 ambapo awali iliitoa Timu ya kituo cha radio cha Triple A, huku timu ya Sunrise Radio ikitoka mapema.

Katika bonaza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, TBL, Kampuni ya simu uya Vodacom,Shirika la hifadhi za Taiga TANAPA, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,Wakala wa simu wa ALPHATEL,NSSF na Cocacola, mgeni rasmi alikuwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye.

Kutokana na ushindi huo, Radio 5 ilipata kombe lenye thamani ya sh.800,000 na fedha taslimu 200,000 ambapo pia Pepsi ilipata kombe lenye thamani ya sh.400,000 na fedha taslim 100,000.

Katika michezo mingine waandishi wa habari wasichana wa Arusha, waliwatambia TASWA Dar baada ya kukamata kuku wawili.

Akizungumza wakati akikabidhi zawadi, Andengenye aliwataka wafadhili zaidi kujitokeza kusaidia bonanza hilo kila mwaka kwani linarejesha mahusiana na kujenga afya kwa wanahabari na wadau wa habari.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates