BREAKING NEWS

Monday, July 25, 2011

MADEREVA DALADALA ARUSHA WAGOMA ,ABIRIA WANAFUNZI WALA MSOTO


wanafunzi wakichangamkoa usafiri wa boda boda ili kuwahi masomo




Mamia ya wanafunzi na baadhi ya wananchi wakiwa wamejikusanya katika barabatra ya uhuru wasijue la kufanya baada ya magari ya daladala kugoma.



madereva hao wanalalamikia mambo mbalimbali ikiwemo adhabu ya kifungo cha siku 14 magerezani mara wanapokamatwa na kwamba wenzao zaidi ya 40 tayari wamehukumiwa kifungo gerezani




Baadhi ya wadereva wa dala dala wakiwemo wapiga debe walilizonga gari aina ya haice ambalo lilionekana likikaidia amri ya kugoma na kuendelea kupakia.

HALI si shwari katika jiji la Arusha mara baada ya jeshi la polisi kuingilia kati na kuzima maandamano ya madereva wa daladala pamoja na makondakta kwa kwafayatulia mabomu ya machozi,walipokuwa wakiandamana asubuhi kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.

Madereva hao wametangaza mgomo usio na kikomo hadi pale madereva wenzao zaidi ya 50 waliopo mahabusu na magereza waachiwe huru bila masaharti yoyote.


Huduma za usafiri jijini Arusha zimesimama tangu majira ya saa 11;00 asubuhi baada ya madereva hao kushinikiza kilio chao kisikilizwe ambapo mojawapo ya madai yao ni pamoja na unyanyasaji kupitia askari wa usalama wa barabarani.


Maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwemo wanafunzi wamelazimika kutembea kwa miguu kwa umbali mrefu kwa zaidi ya kilomita 50 kwenda maeneo mbalimbali katikati ya mji kutokana na mgomo huo hali iliyopelekea madereva wa pikipiki maarufu kama “bodaboda” waliazimika kupakia abiria hao ili kuwafikisha katika maeneo mbalimbali.

Hata hivyo,katika hali isiyo ya kawaida askari wa usalama wa barabarani ambaye hakutambulika jina lake mara moja alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushushiwa kipigo kikali na madereva hao wakiwemo wapiga debe katika eneo la Annex jijini hapa wakati akiongoza magari kitendo kilichopelekea kukimbilia katika duka la kuuza majokufu lililopo mkabala na jengo la Kimahama kwa lengo la kunusuru maisha yake.


Jeshi la polisi lililazimika kuzuia kundi la madereva hao wapatao 200 majira ya saa 4;00 asubuhi katika eneo la mnara wa Mwenge jijini hapa kwa kuwatawanya huku wakitumia mabomu ya machozi zaidi ya 10 hali iliyozua tafrani katikati ya jiji la Arusha na kupelekea shereha za mashujaa zilizokuwa zikifanyika katika ofisi ya mkoa kuingia dosari.


Magari ya jeshi la polisi yakiwa yemesheheni askari wenye silaha na mabomu yalikuwa yakizunguka katikakati ya jiji la Arusha kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao jijini hapa.


Wakizunguza kwa nyakati tofauti madereva wa daladala pamoja na makondakta kwa nyakati tofauti walisema ya kuwa wao wanapinga vikali kitendo cha jeshi la polisi kuwakamata wenzao ambao ni zaidi ya 40 na kwa maksoa ya barabarani na kisha kuwafikisha jela kwa makosa ya ujambazi.

Madereva hao waliwataja askari hao kwa majina ya Modesta,Peter na Dan kuwa wamekuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata mara kwa mara huku wakiwaomba rushwa ya kiasi cha sh,10,000 hadi sh,250,000 kitendo wanachodai sio haki.


Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Arusha,Isdore shirima alitoa tamko la kuwataka madereva hao kurudisha magari barabarani wakati serikali na vyombo husika wakashughulikia suala lao

Katika hatua nyingine mahabusu waliofikishwa mahakamani majira ya saa 5;00 katika mahakama kuu kanda ya Arusha kwa lengo la kusikiliza hatma ya kesi zao waligoma kushuka ndani ya karandiga hilo huku wakidai kuwa kucheleweshwa kusikilizwa kwa keshi zao.


Kizaazaa hicho kiliibuka mahakamani hapo na kuepelekea mahabusu hao kurudishwa rumande baada ya kugoma kushuka katika karandiga hilo ambapo pamoja na juhudi za kuwashawishi kushuka ndani ya karandiga hilo kufanywa lakini waliendelea kugoma .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates