BREAKING NEWS

Friday, July 8, 2011

WATATU WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI TOFAUTI

Watu watatu wamefariki dunia mara baada ya kugogwa na magari katika sehemu tofauti mkoani hapa.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Akili mpwapwa alisema kuwa matukio hayo yalitokea July 7 katika maeneo tofauti ya mkoani hapa ambapo alisema kuwa ajali ya kwanza ilitokea katika maeneo ya Majengo kibaoni ambapo gari lenye namba za usajili T249 AMH aina ya Isuzu Tipa ambalo ni mali ya dayosisi ya mkoa wa Arusha lililokuwa likiendeshwa na Peter Mosi (63)lilimgonga mtoto aliyejulikana kwa jina la Easter Alois mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo mpaka sasa akijabainika na dereva wa gari hilo anashikiliwa na jeshi la polisi mpaka pale upelelezi utakapo kamilika ambapo atafikishwa mahakamani.

Alitaja tukio lingine kuwa lilitokea majira ya saa nne usiku katika eneo la majengo ambapo gari lenye namba za usajili T997 AZQ Toyota gruzer lililokuwa likiendeshwa na Kristofa Mbasha(37)mkazi wa majengo lilimgonga mtembea kwa miguu ambaye alijulikana kwa jina la Atibu Athumani na kumsababishia kifo papo hapo .

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakina julikana na upepelezi unaendelea ilikubaini chanzo cha ajali hiyo na mwili wa mrehemu umeifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mounti meru.

Katika tukio lingine alisemakuwa gari ambalo namba zake hazikuweza kufahamika na dereva wake pia ajafahamika lilimgonga dereva pikipiki aliyejulikana kwa jina moja la Raimond anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka( 20_25)ambaye alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T755 YMH aina maha ambapo alifariki dunia papo hapo.

Alisemakuwa mpaka sasa bado wanaendelea na upelelezi ili kuweza kukamata gari na dereva ambaye alimgonja mwendesha pikipiki huyo na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika huku miili ya marehemu ikiwa imeifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya maunti meru.

Alitoa wito kwa madereva kutumia barabara vizuri ili kueza kuzuia ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara huku akiwasihi watembea kwa miguu kufuata sheria za barabarani.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates