BREAKING NEWS

Friday, July 22, 2011

KATIBU MKUU TFF KUWA MGENI RASMI TAMASHA LA WAANDISHI ARUSHA

KATIBU mkuu wa Shirikisho wa shirikisho la soka nchini(TFF), Angetile Oseah anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la sita la waandishi wa habari Kanda ya kaskazini ambalo litafanyika jumapili viwanja vya General Tyre mjini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Rich Hotel, Katibu mkuu wa TASWA Arusha, Mussa Juma, alisema tayari maandalizi ya Tamasha hilo, yamekamilika na timu za Manyara na jijini Dar es Salaam zinatarajia kuwasili leo Arusha.

Juma alisema katika Tamasha hilo, ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL),Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom, Shirika la hifadhi za taifa(TANAPA),kampuni ya uwakala wa simu ya ALFATEL,NCAA na NSSF jumla ya timu 12 zitashiriki..

Mratibu wa Tamasha hilo, ambalo huandaliwa na TASWA na kampuni ya MS Unique alizijata timu ambazo zinashiriki kuwa ni timu za TASWA Arusha,Taswa Dar,Radio TripleA,Radio 5, Radio Sunrise FM,Chuo cha uandishi habari cha Arusha, Radio ORS ya Terati mkoani Manyara, MJ radio, NSSF Arusha,TBL,Wazee Klabu na PEPSI.
"washindi wa kila mchezo watapatiwa kikombe na fedha taslim na hii ni kuhamasidha wanahabari kupenda michezo"alisema Omar.
Omar alisema tamasha hilo,litapambwa na benki ya watoto wa tembo ikiongozwa na Ndanda kosovo na jioni kutakuwa na hafla ambayo itafanyika Ricks Klabu.
Wakizungumzia Tamasha hilo, Meneja mauzo wa TBL mikoa ya Arusha, Manyara na Singida , Wilderson Kitio na Msimamizi wa mawakala wa Vodacom Kanda kaskazini,Michael Kasubi, walisema wameamua kudhamini tamasha hilo kutokana na kutambua mchango wa wanahabari katika jamii.

Kitio alisema TBL itaendelea kushirikiana na wanahabari katika tamasha hilo kila mwaka ili kuhakikisha wanashiriki vyema katika michezo kwani michezo ni afya, furaha na burudani.
Naye, Kasubi alisema Vodacom kama wadau wa michezo hapa nchini, wanathamini sana mchango wa vyombo vya habari katika jamii na ndio sababu wamekuwa wakijitokeza kila mwaka kushirikiana na wanahabari.
Kwa upande wa TANAPA, Meneja Mahusiano Pascal Shelutete alisema wanahabari wananafasi kubwa ya kutangaza utalii katika nyaja mbali mbali kama michezo ambayo imekuwa ikipendwa na watu waliowengi

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates