BREAKING NEWS

Monday, July 18, 2011

JKT MBWENI YANYAKUA TAJI

Chama cha Netball nchini CHANETA,kimetoa baraka kwa vilabu vya netball kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuinua ari na kuuboresha mchezo huo



Hali hiyo imetokana na mchezo wa netball kuonekana kusuasua katika miaka ya hivi karibuni


Mwakilishi wa kaimu katibu mkuu wa Chaneta Shiza Mwakatundu ametumia nafasi ya kufungwa kwa michuano ya netnball daraja la kwanza iliyomalizika jijini Arusha kwa kubainisha kuwa ,wachezaji wa kigeni watasaidia kuinua ari kwa wadau wa netball kuupenda mchezo huo



Shiza amesema,mashindano ya mwaka huu hamasa imeongezeka kutokana na baadhi ya timu kusajili wachezaji kutoka nje hali iliyowafanya wachwezaji wa hapa nchini kujifunza mengi kutoka kwa wachezaji hao.


"vilabu vingi vimeleta wachezaji kutoka nje hali ina;yosabisha wachezaji wetu kupata kuiga baadhi ya mambo yao ya kimichezo pamoja na kujifunza mengi kutoka kwao"alisema Shiza Mwakatundu



Mkuu wa wilaya ya Arusha aliyekuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mashindano hayo Raymond Mushi,ameupongeza uongozi wa CHANETA kwa kuona umuhimu wa mashindano ya daraja la kwanza kufanyika jijini Arusha



Mkuu huyo wa wilaya ametumia nafasi hiyo kuwanyooshea kidole wachezaji kujikinga na maambukizi ya ukimwi huku mfungaji bora wa mashindano hayo Mwanaidi Hassan kutoka timu ya JKT Mbweni akibainisha kuwa wana uhakika wa kufanya vizuri katika michuano ya muungano na ile ya Afrika Mashariki



Katika michuano hiyo iliyoanza July 3 na kufikia ukingoni July 16 kwenye uwanja wa Shekh amri Abeid timu ya JKT Mbweni imefanikiwa kutetea taji lake kwa kushika nafasi ya kwanza



Timu ya Filbert Bayi imeshika nafasi ya pili,Jeshi Stars imeshika nafasi ya tatu na nafasi ya nne imechukuliwa na Magereza Morogoro



Tuzo ya mchezaji bora imechukuliwa na Takondwa Lwazi wa Zimbabwe anayechezea timu ya Filbert Bayi wakati tuzo ya mfungaji bora imenyakuliwa na Mwanaidi Hasasan wa JKT Mbweni.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates