BREAKING NEWS

Monday, July 4, 2011

LIGI DARAJA LA KWANZA NETBALL YAANZA POLISI ARUSHA ,MAGEREZA WAANGUKIA PUA


kikundi cha ngoma cha Jkt Oljoro kikitumbuiza na kwaya





Timu ya polisi Arusha ya mchezo wa netball ambayo inashiriki katika mashindano ya ligi daraja la kwanza ngazi ya taifa imeangukia pua mara baada ya kutandikwa magoli 13-12 na wapinzani wao ambao ni timu ya Polisi morogoro katika mechi yao ya ufunguzi wa mashindano hayo waliyoicheza katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Timu hiyo ambayo ndiyo wenyeji wa mshindano haya ilionekana kulemewa na mchezo huu hali iliyosababishia timu pinzani ambao ni polisi morogoro kujipatia magoli mengi katika kipindi cha kwanza.

katika kipindi cha kwanza timu ya Polisi morogoro ilianza kuingiza goli la kwanza katika pete na iliweza kuongoza katika kipindi chote chakwanza hali ambayo ilisababisha hadi kipenga kupulizwa timu ya Arusha kuambulia magoli sita huku timu ya morogoro ikiambaulia magoli tisa,katika kipindi cha pili timu polisi Arusha walionekana kuja na kasi kubwa na kusabisha kuweza kujipatia magoli ya harakaharaka hali iliyosabisha hadi kipenga cha mwisho kupulizwa timu ya morogoro kuongoza na goli moja wakiwa na wanamagoli 13 huku Arusha walikiwa na magoli 12.

Gazeti hili lilizungumza na kocha wa timu ya polisi Arusha Josephu Lameck (Dudu) alisema kuwa wamefurahia mchezo ila wamechukizwa sana na waamuzi wa mchezo huo kwani walikuwa wanapendelea timu moja.

"jamani naweza sema kuwa waamuzi hawa hawakuchezesha mchezo kwa usawa kwani walikuwa wanapendelea upande mmoja sana walishindwa kumiliki mchezo ,ila pamoja na yate hayo naweza sema tumeshinda maana tumecheza na timu kubwa sisi tumepanda daraja juzi wao ni wakongwe na wanashikilia nafasi ya tatu katika ubigwa wa taifa ivyo naweza kujisifu kwa hilo kwakeli tume jitaidi"alisema Lameck(dudu).

Alibaindish kuwa mbali na hilo pia timu yake bado ilikuwa inaouwaga mkubwa katika mechi hile kwani ilikuwa haijawai kucheza mechi ya kirafiki hata moja tangu walivyo anza kambi kwa hiyo ilikuwa haijakomaa vyema na hiyo ndio sababu ingine iliwaafanya wakashindwa kutoka kidedea na hii pia ilisababishia kupoteza mipira mingi katika kipindi cha kwanza.

Kwa upande wake kamanda wapolisi wa mkoa wa Arusha ambaye ni mlezi wa timu polisi Arusha Thobias Andengenye aliliambia gazeti hili kuwa mashindano haya ni mazuri na yanamsisimko pamoja kuwa wenyeji hawajaanza vizuri sana ila wamejitaidi kucheza kwani wamecheza na timu kubwa lakini wameweza kutoka tofauti ya goli moja.

Alisema kuwa wanauwakika kabisa katika mechi ambazo zitafuata timu ya polisi Arusha itashinda kwani watakuiwa wameshazoea wachezaji na mchezo na wanahaidi kubalikiza kombe la mchezo wa netball mkoani hapa.

Alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa mchezo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ya mkoa ili iweze kupata morali ya kucheza vyema katika mashindano haya.

Katika mechi ingine mabigwa watetzi JKT Bweni waliweza kuibuka kidedea mara baada ya kuwafunga timu ya Magereza morogoro magoli 33 -18 mechi ambayo ulikuwa ya kusisimua kwani timu zote zilikuwa zinajiweza.



baadhi ya timu shiriki zikiwa zimepanga foleni mbele ya mgeni rasmi

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates