BREAKING NEWS

Friday, July 8, 2011

KILO 347 ZA MIRUNGI ZAKAMATWA

Jeshi la polisi mkoani hapa limewakamata wafanyabiashara 12 wakiwa na viroba 40 vya Mirungi ambavyo vina uzito wa kilo 347 .

Akiongea na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Akili Mpwapwa alisema kuwa jeshi hilo liliwakamata watu hao ambao wanadaiwa kufanya biashara haramu ya mirungi mara baada ya kupata taarifa kuhusiana na kuwepo kwa watu wa aina hiyo kutoka kwa wasamaria wema.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe saba mwezi wa saba mwaka huu majira ya saa5:00 Asubuhi katika maeneo ya sombetini ndani ya halimashauri ya jiji la Arushaambapo jeshi la polisi lilipata taarifa kuwa gari lenye namba za usajili T292 BDF aina ya Noah lililokuwa linatokea Ngaramtoni kuelekea mjini limebeba mihadarati ambayo ni mirungi.

Alisema kuwa baada ya polsi kupata taarifa hizo walianza kufuatilia gari hilo kwa nyuma na kuona linaingia katika mtaa huo wa sombetini katika nyumba ya Mwananchi aliyemtaja kwa jina la Mohamed Salmada .

"baada sasa ya polisi kuona gari hilo limeingia katika nyumba hiyo walishuka na kwenda moja kwa moja kugonga katika mlango ambao gari lile liliingia mara baada ya kuona polisi watu wale waliamua kuanza kutoa mirungi hilo kwa kupitia dirisha la nyuma na kupeleka mirungi ile nyumba ya pili "alisema Mpwapwa.

Alibainisha kuwa mara baada ya polisi kugundua mbinu ile walizingira nyumba yote na ndipo wakawakamata wafanyabiashara hao 12 waliokuwa wakifanya shuhuli ya kuamisha mirungi iyo.

Aliwataja watu hao waliokamatwa kuwa ni Mohamed Salmada (39)Mdigo mfanyabiashara na nimkazi wa Sombetini,Kasimu Mohamed(42),Loswita Benjamin (30),Fatuma Iddi(42),Hadija Ramathadhani(43),Lena JOhn (25),Asia Said,Teddy Komba(42),Mayasa Ngoya (32),Khadija Issa(38),Salimu Ally(28) pamoja na Zanila Salimu (30)wote wakiwa ni wafanyabiashara wa mirungi.

Alisema kuwa mpaka sasa mmiliki wa gari hilo lililokuwa limebeba mirungi hiyo ajapatikana na watuhumiwa wanashikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kutoa taarifa za uhalifu pindi tu wanasikia unataka kutokea na watoe taarifa za sehemu zozote ambazo wanasikia kuna mihadarati ya aina yoyote.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates