BREAKING NEWS

Wednesday, July 27, 2011

U-23 WAILIZA SEYCHELLES




picha ikionyesha mchezaji wa timu ya Tanzania ya U-23 Jamal Mnyata akiwa anajaribu kumponyoka beki wa timu ya Seychelles Bibi Jonathan katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid


Mshambuliaji chipukizi wa timu ya taifa ya vijana Thomas Ulimwengu amefunga hati triki kuongoza timu ya vijana U-23 mara baada ya kuizamisha timu ya taifa ya Sheli sheli (Seychelles)mgoli matatu kwa limoja.

Ulimwengu alianza kuesabu goli la kwanza katika dakika pili ya mchezo mara baada ya kupokea pasi kutoka kwa mchezaji Salumu Machaku kabla ya kuongeza bao la pili katika dakika ya 49 kufuatia piga nikupige liliklotokea katika lango la timu ya Sychelles lililotkana na kona ya Salumu Machako.

Nyota Thomasi Ulimwengu ilizidi kungara katika dakika ya 61 ya kipindi cha pili pale alipoipatia timu ya taifa ya vijana U-23 goli la tatu baada ya kugonga vyema kati ya Juma seif Kijiko na Jamal Mnyate.

Kwa upande wa timu ya Seychelles walipata goli lao pekee ktika dakika ya 34kupitia kwa mchezaji wao Laruu Allen baada ya mabeki wa timu ya taifa ya vijana U-23 kuzembea kuokoa mpira katika eneo la hatari.

Kocha wa timu ya vijana aliwatoa wachezaji watatu kwa mpigo Thomas Ulimwengu ,Salumu Machaku na Babu Ally ambapo nafasi zao zilichukuliwa na wachezajiHussen Javu,Hamis Mcha pamoja na Salum Kanoni.

mara baada ya mechi kumalizika gazeti hilililifanya mahojiano na kocha wa timu ya Tanzania U-23 Jamhuri Kihwelo naye alisema kuwa ushindiwake umepatikana kutokana na timu yake kuwa nzuri pamoja na vijana wake kujianimini,

"mimi naweza sema kuwa ushindi wetu umetokana na sisi wenyewe kuweza kujiamini vijana wangu wanajiamini sana na wanachezaga kwa nguvu zote pale ambapo wanapo kuwa wanacheza timu kubwa huwaga wanatumia nguvu zaidi pia kuwepo kwa kocha wa timu ya taifa imewaongezea vijana morali ya kucheza"alisema Jamhuri.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates