BREAKING NEWS

Saturday, July 30, 2011

Flag this message WATUMISHI WA HOTELI KUBORESHEWA MASLAHI YAO.

UONGOZI wa hoteli ya kitalii yenye hadhi ya nyota nne ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha umeweka mkakati maalumu wa kuanza kuboresha maslahi ya watumishi wake kwa lengo la kukuza ubora wa hoteli hiyo katika medani ya kimataifa.

Pia umejipanga kuboresha utashi wa huduma zinazotolewa hotelini hapo ikiwa ni pamoja na kuwapandisha vyeo baadhi ya watumishi wake wanaofanya juhudi kazini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mkoani Arusha na afisa mahusiano wa hoteli hiyo,Mariki Theron alisema ya kuwa ubora wa hoteli yoyote duniani unategemea maslahi mazuri ya watumishi wake hivyo na wao wamejipanga kujikita katika eneo hilo.

Alisema ya kuwa uongozi wa hoteli hiyo umeshaweka mikakati ya kuwekeza kwa watumishi wake ambapo eneo mojawapo ni watakaloliangalia ni kuboresha maslahi ya watumishi wake kama kupandisha mishahara na kuongeza malipo ya muda wa zaida.

“Tumejipanga kuboresha utashi wa hoteli yetu kwa kutoa huduma zake mahiri hii ni pamoja na kuwekeza katika nyanja ya kuboresha maslahi ya watumishi wetu”alisema Mariki

Alibainisha ya kuwa katika mkakati huo pia wamejipanga kuwapa motisha watumishi mbalimbali wa hoteli hiyo ambapo kwa sasan mtumishi yoyote atakayeonyesha juhudi bora kazini watampandisha cheo na kumpatia zawadi mbalimbali kama kutambua mchango wake kazini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya watumishi wa hoteli hiyo,Rodney Rugambo,Chief Conciege,Ben Gitariga,Michael Kimaro na Frida Khatibu walionyeshwa kufurahishwa na hatua za uongozi wa hoteli hiyo huku wakihaidi kutoa ushirikiano wa dhati katika kukuza ubora wa hoteli hiyo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates