BREAKING NEWS

Thursday, July 28, 2011

WANAFUNZI WAKATISHA MITIANI KISA UMEME

CHUO kikuu cha Arusha(UOA) kampasi ya Arusha mjini kimelazimika kukatisha mitihani yake mara kwa mara kutokana na tatizo la mgao wa umeme unaolikumba taifa katika kipindi hiki hali ambayo imekuwa ikichangia kudhorotesha masomo kwa wanafunzi chuoni hapo.

Pia, wanafunzi wa chuoni hapo mara nyingine wamelazimika kutumia mwanga wa tochi kujisomea katika vyumba vyao vya madarasa nyakati za jioni hali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kwa wanafunzi hao chuoni hapa.

Hayo yalisemwa na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo katika makabidhiano ya jenereta lililotolewa hivi karibuni kama msaada na raia wa nchini Marekani,Koffi Okyere ambapo jumla ya kiasi cha sh,800,000 zimegharimu kununulia jenereta hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi chuoni hapo,Elinami Peter na Robert Guemelo walisema kuwa tatizo la mgao wa umeme chuoni hapo limekuwa ni kero na kilio kwao kwa kuwa wamekuwa wakikatisha mitihani yao ambayo hufanywa nyakati za jioni kutokana na kukosekana kwa nishati ya umeme chuoni hapo.

Walisema mara nyingine wamekuwa wakilazimika kutumia mwanga wa tochi darasani mwao kumulikia vitabu vyao kutokana na giza totoro nyakati za jioni linalotokana na kukosekana kwa nishati ya umeme hali ambayo imekuwa ni kikwazo kwao.

Mwanachuo mwingine chuoni hapo,Karem Benjamin alisema kuwa kupatikana kwa jenereta hilo chuoni hapo kutapunguza kero ya uhaba wa nishati ambayo walikuwa wakiipata kwa muda mrefu huku akiitaka serikali hapa nchini kutatua tatizzo la mgao huo kwa kuwa linaathiri sekta ya elimu hapa nchini.

Naye,makamu wa mkuu wa chuo hicho,Dk Laban Irhene alisema kuwa kuwa ni faraja kupatikana kwa jenereta hilo kwani limekuja katika kipindi mwafaka huku akimshukuru Prof,Okyere kwa kulichukulia tatizo la uhaba wa nishati chuoni hapo kama tatizo lake binafsi.

Aliitaka serikali kutatua tatizo la mgao wa umeme hapa nchini kwa uharaka na kusisitiza kuwa endapo serikali ikizembea kuchukua hatua huenda likaathiri uchumi wa nchi kuporomoka kwa kasi pamoja na sekta binafsi kuathirika kwa wingi.

"Tusiporekebisha tatizo hili litaleta madhara makubwa kiuchumi na utaporomoka kweli kweli na ni ngumu kuinua uchumi ulioporomoka,hili tatizo huenda baadaye likawa janga la kitaifa"alisema Irhene

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates