BREAKING NEWS

Monday, July 18, 2011

TAMASHA LA FIESTA WATATU WACHOMWA VISU ARUSHA

Watu watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya katika tamasha la muziki la Fiesta lililiofanya juzi katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid jijini hapa.

Watu hao watatu wameumia baada ya kuchomwa visu katika katika tamasha hilo, ambalo lilifurika vijana wengi pamoja na watoto na baadae kufumuka vurugu.



AKiongea na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema kuwa matukio hayo yalitokea wakati tamasha hilo la mziki likiendelea, ambapo kulikuwa na vijana wengi wa kihuni waliohudhuria tamasha hilo .



Aliwataja watu hao wealiojeruhiwakwa kuchomwa visu kuwa ni Mustafa Salumu (20), aliyejeruhiwa vibaya katika mkono wake wa kushoto. Hata hivyo, hakumjua mtu aliyemchoma kisu hicho kwani baada ya kumchoma alitokomea katika kundi la watu.


Alimtaja mtu mungine aliyejeruliwa kuwa ni Ally Kassimu (23) mkazi wa Ungalimitedi ambaye alichomwa kisu cha mgongoni na mtu aliyemtaja kwa jina la Geodratus Leakimu (25), ambaye ni mkazi wa Lemara mjini hapa.

"Sasa huyu Ally wakati anachomwa kisu bahati nzuri maaskari waliweza kumuona mtu aliyemchoma hivyo wakamshika na mpaka sasa anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani muda wowote upelelezi utakapokamilika, “alisema Mpwapwa.



Alimtaja mwingine aliyejeruhiwa kwakisu kuwa ni Saidi Juma ambaye yeye alichomwa kisu cha mbavu na mtu ambaye hajaweza kufahamika jina lake kutokana na vurugu na wingi wa watu waliokuwepo uwanjani hapo.



Alisema kuwa watu hao baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa waMaount Meru, waliruhusiwa kwa nyakati tofauti, lakini Juma bado amelazwa katika hospitali hiyo akiendelea na matibabu.



"Unajua hili tamasha sawa ni zuri, lakini kiukweli sijui maana yake naweza kusema nila kihuni maana jana watu walijaa sana uwanjani na wengi waliibiwa simu walipigwa pamoja ya kuwa taarifa tulizoripotiwa ni hizo, lakini wengi walipata matatizo, “alisema.



Kamanda huyo alitoa wito kwa waandaaji wa tamasha kama hili kujitahidi kuweka japo ulinzi wa hali ya juu ili kuweza kuzuia fujo ambazo zinatokea na saa nyingine waweke kiingilio cha juu ili kuweza kuwazuia vibaka pamoja na watu ambao wanakuja kuingia kwa niaya fujo pamoja na wizi kutoingia.

Naye Kamanda wa polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Zuber alisema kuwa wao kama jeshi la waliyoa ulinzi wa kawaida, lakini kutokana na jinsi watu wilivyozidi kuongezeka ilibidi wazidi kuongeza ulinzi zaidi.

Alisema kuwa tamasha hilo lilikuwa na vijana wengi wa kihuni, hali iliyowafanyawa polisi kujaribu kutumia nguvu zaidi ili kujaribu kuthibiti fujo hizo.



"ilifikia mahali ikabidi nitafute wale watu wetu wa polisi jamii ili waweze kuwasindikiza watu na wengine kuwalinda watu maana kulikuwa na vijana ambao wamekunywa pombe wanaleta fujo za ovyo, “lalisema OCD Zuberi

Alisema pia anapenda kuwahasa akina mama waliokuja na watoto kutofanya hivyo kipindi kingine, kwani jinsi wanavyokuja na watoto wanaweza kupata mathara katika fujo hizo zinazotokea usiku.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates