BREAKING NEWS

Saturday, July 2, 2011

WAPATIWA CHAKULA CHA MSAADA

Ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa kimetola tani za 1,300 za mahindi kwa wakazi wa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya kuwagawia wakazi wa wilaya hiyo ambao wamekubwa na tatizo la njaa pamoja na wale ambao wamepungukiwa na chakula.

|Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya hiyo Khalid Juma Mandia,wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani humo.

alisema chakula hicho kitatolewa kwa wakazi wote wenye upungufu wa chakula katika vijiji vyote vya wilaya hiyo.

Mandia alisema hali ya ukame katika wilaya hiyo imeathiri upatikanaji wa mazao ya chakula,hivyo anaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwapatia chakula hicho cha msaada wa njaa.

Aidha alibainisha kuwa mwezi Mei mwaka huu,Serikali iliipatia chakula wilaya hiyo kiasi cha tani 601 za mahindi na wakazigawa kwa wananchi wenye upungufu wa chakula katika vijiji 28 vya kata mbalimbali za wilaya ya Simanjiro.

“Kwa niaba ya wakazi wa Simanjiro,nachukua nafasi hii kuishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa kwa kutupatia chakul kwani kitasaidia kuwasukuma wananchi katika tatizo la njaa,” alisema Mandia.

Alisema kuwa katika wilaya ya Simanjiro,hivi sasa hakuna kijiji kilicho na hali nzuri ya chakula,kutokana na ukame uliokuwepo na kuathiri mazao yaliyolimwa ambayo yalikaukia mashambani .

Alisema kwenye wilaya yake,hali ya hewa mwanzoni ilikuwa nzuri baada ya mvua kunyesha na wakulima kupanda mazao yao mashambani,lakini ghafla ilibadilika na kuathiri kwa kiasi kikubwa mazao yaliyokuwepo
mashambani.

Mkuu huyo wa wilaya alisema mchakato wa zoezi la kugawa chakula hicho umeanza rasmi kwa kuandaa magari yatakayosambaza chakula hicho kwenye vijiji vyote vya wilaya hiyo.

“Katika ugawaji wa mahindi hayo wale wenye upungufu wa chakula watanunua kila kilo moja kwa sh50 na pia watu kama vikongwe,walemavu na wale wasiojiweza watapatiwa chakula hicho bure,” alisema Mandia.

Aliwataka viongozi wote wa vijiji hivyo kugawa chakula hicho kwa utaratibu mzuri na endapo itabainika kuna kiongozi amejinufaisha yeye binafsi kwa kujigawia mahindi hayo atamchukulia hatua kali za kisheria.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates