BREAKING NEWS

Wednesday, July 20, 2011

NDANDA KOSOVO KUPAMBA TAMASHA LA WAANDISHI ARUSHA



mwanamziki Ndanda Kosovo akiwa na waimbaji wake wakati wakiimba mbele ya waandishi wa habari ambapo wanatarajiwa kupamba tamasha lao linalofanyika jumapili July 24 katika viwanja vya General Tyre mkoani hapa


wa kwanza kushoto ni meneja wa mawakala wa kampuni ya simu ya vodacom Maico Kasubi akifuatiwa na mratibu wa tamasha hili la waandishi Jamila Omari ,huku wa kwanza kushoto ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha (Taswa Arusha) Mussa Juma akifuatiwa na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini TBL Wilderson Kitio wakati walivyo fanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Richi hotel jijini hapa kuhusiana na tamasha hilo waandishi wa habari


TAMASHA la sita la vyombo vya habari Kanda ya kaskazini linatarajiwa kufanyika julai 24 katika viwanja vya General Tyre Arusha.


Akiongea na waandishi wa habari mratibu wa Tamasha hili Jamila Omary alisema kuwa tamasha hili huandaliwa kila mwaka na TASWA Arusha na kampuni ya MS Unique promotion ya Arusha, litashirikisha timu za waandishi wa habari toka mikoa ya Arusha, Manyara na Jijini Dar es slaam.


Alisema kuwa Katika tamasha hili, kutakuwa na michezo ya soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku,mpira wa pete na mbio za magunia.


Mgeni rasmi katika tamasha hili anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Isdore Shirima pia kutakuwa na bendi ya Watoto wa Tembo ikiongozwa na Ndanda Kosovo siku ya tamasha.


Timu zitakazo shiriki katika tamasha hili ni TASWA Arusha,Taswa Dar,Radio TripleA,Radio 5, Radio Sunrise FM,Chuo cha uandishi habari cha Arusha, Radio ORS ya Terati mkoani Manyara,NSSF Arusha,TBL,Wazee Klabu na PEPSI.


Tamasha hili limedhaminiwa na Kampuni ya bia nchini, TBL, kampuni ya simu ya Vodacom, TANAPA,mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,NCAA, ALPHATEL, NSSF

Baada ya tamasha kutakuwa na hafla ambayo itafanyika Ricks klabu Philips kuanzia saa moja usiku hadi asubuhi


Kwa upande wa meneja mauzo wa kampuni ya bia ya TBL kanda ya kaskazini Wilderson Kitio alisema kuwa wao wameona umuhimu wa michezo ndio maana wameamua kuthamini tamasha hili.


Aliongeza kuwa pia wameamua kuwapa ushirikiano waandishi wa habari kwakuwa na wao wamekuwa wakiwapa ushirikiano katika mambo mbalimbali.


Alitoa wito kwa wapenzi wa michezo na wapenzi wa wanahabari wajitokeze kusherekea kwa pamoja katika tamasha hilo ambalo wameliandaa kwa ajili ya kujumuika pamoja.


Kwa upande wake meneja wa mawakala wa kanda ya kaskazini wa kampuni ya vodacom Maico Kasubi alisema kuwa wamefurahia sana kwa waandishi wa habari kutambua umuimu wao na kuwaruhusu kushiriki kwa pamoja katika tamasha hili.


Alitoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza katika tamasha hilo ambalo alisema waandishi wa habari wameandaa mambo mengi ikiwemo msaanii ambaye makazi yake ni mkoa wa arusha ajulikanae kama ndanda kosovo ambaye atakuwa na bendi yake ya watoto wa tembo

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates