BREAKING NEWS

Monday, July 18, 2011

WATAKIW A KUFUNGUA MIPAKA

Serikali imetakiwa kufungua mipaka yote ya kuuza mazao ya chakula ili wakulima waweze kunufaika na kilimo chenye tija kwani kufungwa kwa mipaka kutasababisha wakulima wengi kukata tamaa ya kulima mazao mengi.

Hayo yalielezwa na mwanachama na mjumbe wa bodi ya mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) Rehema Mwateba wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wanne wa Taasisi ya wakulima wadogo Tanzania (Mviwata) ikishirikisha wanachama wa Wilaya tano za mkoa wa Manyara.

Mwateba alisema Serikali itambue kwamba imetumia mfumo kandamizi kwa mkulima kufunga mipaka ya kuuza mazao ndani na nje ya nchi bila yakujali kuwa hitaji la mkulima la kuendesha maisha yake yanayotegemea bei nzuri ya mazao.

“Serikali inatakiwa kutoa fedha kwa ajili ya kilimo kwanza na kufanya utafiti wa haraka kwa maeneo yaliyoathirika na njaa na kupeleka chakula cha msaada na maeneo mengine yasiokuwa na uhaba wa chakula na kuruhusu kuuza mazao yao nje ya nchi ili kuweza kupata fedha nyingi,” alisema.

Makamu mwenyekiti wa Mviwata Mkoa wa Manyara,Fatuma Kimolo alisema kama serikali imeamua kufunga mipaka ya kuuza chakula inatakiwa sasa ijipange kununua mazao hayo ya wakulima kwa bei yenye tija badala ya kupanga bei yao wenyewe isiyokuwa na maslahi kwa mkulima.

Kimolo alisema kufuatia kufungwa mipaka hata bei ya mazao ya mahindi yameshuka kwani awali gunia moja la mahindi lilikuwa likizwa kwa sh 45,000 na sasa sh30,000 kwa gunia moja hali ambayo imeonekana kurudisha maendeleo ya mkulima.

Alisema watumishi wa Serikali wamekuwa wakipandishwa mishahara kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha ili yaweze kuwa rahisi lakini wamemsahau mkulima nae anahitaji kuuza mazao yake kwa bei ya juu ili aweze kukabiliana na maisha magumu.

Aliiomba Serikali iache kutoa matamko ambayo hayana tija kwa ustawi wa wakulima na ukuaji wa nchi katika bishara za kimataifa na kutotumia nguvu kubwa za dola kuzuia wanaovusha mahindi badala yake waimarishe miundombinu ya kilimo ili kiweze kuwa na uzalishaji wa kutosha hadi kuuza nje ya nchi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates