BREAKING NEWS

Saturday, July 2, 2011

LIGI DARAJA LA KWANZA NETBALL KUANZA KESHO

Wadau mbalimbali wa michezo wa mkoa wa Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mashindano ligi daraja la kwanza ya mchezo wa pete yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Leo(kesho) katika uwanja wa kumbukumbu za Sheikh Amri Abeid jijini hapa .

Akiongea na gazeti hili msimamizi wa mashindano haya ambaye pia mjumbe wa kamati kuu CHANETA Mwajuma Kisembo alisema kuwa mashindano haya yanatarajiwa kuanza kesho rasmi na yatafunguliwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Raimondi Mushi.

Alisema kuwa walikuwa wanatarajia timu 20 kushiriki katika mashindano haya lakini hadi sasa ni timu 17 tu ambazo zimethibitisha kushiriki mashuindano haya na zimeshawasili mkoani hapa kwaaajili ya mashindano.

Alizitaja timu hizo kuwa ni Polisi Mbeya ,Polisi Morogoro,Polisi Dar es salaam,Filbert Bayi, Jeshi Stars,JKT Mbweni, Mapinduzi Dodoma,Polisi Pwani,Hamambe Mbeya,Magereza Morogoro, Polisi Mwanza pamoja na Uhamiaji Makao makuu.

Timu nyingine ni JKT Ruvu, Tamisemi,CMTU,Tumbaku Morogoro,Polisi Mbeya pamoja na wenyeji wa mashindano hayo ambao ni Polisi Arusha.

"timu zilizofika ndo hizo ila kuna timu tatu ambazo hazitashirikil mashindano haya kutokana na matatizo tofauti tofauti ambapo timu ya F11 wao wanasababu maalumu ambayo imewafanya wasishiriki,Ras lindi wao wanauhaba wa fedha ambapo ndio sababu imefanya wasishiriki pamoja na Alayance wao bado hawajatoa sababu maalumu ya kutoshiriki mashindano haya"alisema Kisembo.

kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha CHANETA mkoa wa Arusha Mercy Rwezaura alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na mashindano haya yataanza rasmi Leo(kesho) na kwa siku ya kesho jumla ya mechi mbili zitacheza lakini kuanzia siku inayofuata kila siku kutakuwa na mechi 12 ambazo zitachezwa sita asubuhi na sita mchana.

Alisema kuwa wamefurahia sana mashindano haya kufanyika mkoani hapa kwani ni mda mrefu umeisha tangu mashindano ya mchezo wa pete kama haya kufanyika hapa kwani mashindano ya mwisho yalifanyika 2008.

"kweli watu wa mikoani tumelalamika sana kutokana na mashindano kama haya kutofanyika mkoani hapa sasa tumeletewa katika mkoa wetu sisi ndo wenyeji wa mashindano haya hivyo nawaomba wadau wa michezo wa mkoa huu wajitokeze kushangilia timu yao ya polisi ambayo nayo inashiriki mashindano haya "alisema Rwezaura.

Aidha alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakijitokeza kuangalia michezo kama vile ya mpira wa miguu na kusahau mpira wa pete kitu ambacho sio kizuri kwani mchezo wa pete pia ni mchezo kama michezo mingine .

Rwezaura aliwataja wathamini wa mashindano haya kuwa ni chama cha mchezo wa netball Tanzania (CHANETA) ambao ni wathamini wakuu ambapo pia alisema kuwa kuna wathamini wengine ambao wamejitokeza kuthamini mashindano haya kwa kutoa vifaa ambapo alisema kuwa kampuni ya simu za mkoanoni Vodacom wao wamejitolea kufanyia ukarabati viwanja huku kampuni ya bonete kupitia kinyaji cha maji ya kilimanjaro kutoa maji kwa timu zote shiriki.

"napenda kuwasihi wadau wa soka wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya kwani kwa sasa yanafanyika hapa hapa nyumbani na pia waje waipe nguvu timu yao ambayo inawakilisha mkoa timu ya polisi Arusha iliiweze kufanya vyema "alisema Rwezaura

Mashindano haya yanatarajiwa kufanyika mkoani hapa kwa takribani wiki mbili katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates