BREAKING NEWS

Friday, July 8, 2011

MASHINDANO YA ROLING STONE KUANZA RASMI KESHO

Mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama Roling stone yanatarajia kuanza kutimua vumbi kesho katika uwanja wa Kumbukumbu za Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa.

Mashindano haya yanayoshirikisha timu mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi yanafanyika kila mwaka na haya ni mashindan ya 12 kufanyika mkoani hapa.

Akiongea na gazeti hili kaimu mwenyekiti wa Taasisi ya kuinua vipaji vya vijana Roling Stone Asha Mtumwa alisema kuwa mashindano haya yanatarajia kuanza july 8 na yanashirikisha nchi tano .

Alitaja nchi hizo kuwa ni Burundi ,Kenya ,Kongo,Uganda pamoja na wenyeji Tanzania ambapo alisema kuwa kila nchi inatoa timu za vijana ambao watashiriki katika umri tofauti tofauti ikiwemo timu za U-12,U-15 pamoja na U-20.

Alitaja baadhi ya timu ambazo zinashiriki mashindano haya kuwa ni timu yaSimba ,Timu ya Yanga,Azam,Flamingo,JKt Ruvu,Mbeya Art,Jkt oljoro,Saadan ya bagamoyo, Mwanza united,timu kutoka Burundi,timu kutoka Kongo,timu kutoka Uganda pamoja na timu ktoka Kenya.

"Mashindano haya yatachezwa kwa mfumo wa ligi na yanatarawa kuchezwa kwa muda wa siku mbili kumi na mbili na kila timu ambayo itashinda katika mashindano haya itaondoka na kombe.

Alisema kuwa nia haswa ya mashindano haya ni kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana kama vile taasisi yao ilivyojipanga kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto na vijana.

Asha alisema kuwa mgeni rasmi wa mashindano hya anatarajiwa kuwa katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela

Alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka wa mkoa wa Arusha na wa Tanzani akwa ujula kujitokeza kuthamini mashindano haya kwani alisema kuwa mpaka sasa hawajapata wathamini zaidi ya TFF ambao wamejitolea kuthamini michezo hii kw auchache.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates