Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia |
Waandishi wa habari mkoani Tanga
wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Mbaruku Yusuph wa Gazet la Tanzania
Daima,Amina Kingazi wa Gazeti la The Guardian mkoani Tanga,Burhan Yakub
wa Mwananchi
Sehemu ya waandishi wa habari
mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kulia ni Sussan Uhinga wa gazeti
la Mtanzania Tanga,Pamela wa Tanga One Blog wakifuatilia
Mwandishi wa gazeti la
Habari Leo mkoani Tanga Anna Makange akiuliza swali kwenye mkutano
huo
Mwandishi wa Clouds TV
Mkoani Tanga Gift Kika akiuliza swali kwenye mkutano huo kulia ni
Amina Omari wa gazeti la Mtanzania
Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Anna Abdallah wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu ufunguzi rasmi wa soko la Korosho msimu wa mwaka 2017/2018.
"Niseme tu bei hii elekezi ya korosho imetangazwa na bodi hiyo kwa mamlaka waliopewa chini ya kifungu cha 5(3)(d) ambapo bei hiyo imefikiwa baada ya utafiti wa kupata gharama halisi za kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi na kuongeza asilimia 20 kama faida ya mkulima "Alisema.
Alisema kwa msimu huu gharama ya kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi ni 1,208.39 na asilimia 20 ya faida kwa kilo ni sh.241.68 .
Aidha alisema katika mjengeko wa bei ya korosho ghafi msimu wa 2017/2018 ambapo magunia na kamba vitatolewa na serikali kupitia CBT huku chama cha msingi kikipata sh.90.00,Halmashauri ya wilaya ikipata asilimia 3 ya sh.43.50,mfuko wa wakfu ukipata sh.10.00 ambapo jumla ya gharama ni 143.50 wakati bei elekezi ikiwa ni 1,450.00 na mjengeko wa bei ukiwa ni tsh.1,593.50.
Aliongeza kuwa katika msimu wa ununuzi wa korosho 2017/2018 utafunguliwa rasmi Octoba Mosi mwaka huu huku akiwahimiza wadau wote wanaohusika na uuzaji na ununuzi wa zao la korosho kukamilisha maandalizi ya msimu kabla ya ununuzi kuanza.
"Wadau hao ni pamoja na Sekretarieti za mikoa,halmashauri za wilaya,Wakulima,Vyama vya Ushirika vya Msingi,Vyama Vikuu vya Ushirika,Wakala wa Vipimo,Bodi ya Leseni za Maghala,Waendesha Maghala,Wasafirishaji,Wanunuzi,Mamlaka ya Bandari,Mabenki na wengine ambao wanahusika kwa namna moja au nyengine"Alisema.
Akizungumzia suala la utoaji wa leseni za ununuzi wa korosho, Mwenyekiti huyo alisema bodi hiyo inatumia fursa hiyo kuwahamasisha wanunuzi wa zao hilo wa ndani na nje kuomba leseni ya ununuzi kwa ajili ya msimu wa 2017/2018.
"Leseni hii itatolewa bila malipo yeyote,Fomu namba 2 ya maombi ya leseni za ununuzi wa korosho ghafi inapatikana kwenye tovuti ya bodi ya korosho Tanzania (www.cashew.go.tz) na kwenye ofisi zake zilizopo Mtwara(Makao Makuu) na kwenye matawi yake ya Dar es Salaam,Tanga na Tunduru "Alisema
Hata hiyo alisisitiza umuhimu wa wauzaji,wanunuzi na wadau wa korosho kufuata mfumo wa stakabadhi ghalani wa kuuza na kununua korosho huku akitoa wito kwa yeyote atakayekiuka sheria,kanuni na mwongozo namba 1 wa mwaka 2017/2018 wa mauzo ya korosho,atachukuliwa hatua kali ikiw ni pamoja na kutaifishwa korosho.
Habari kwa hisani ya Blog ya
Kijami ya Tanga Raha
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia