Mkuu
wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akionyesha eneo la mradi
litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge
Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme.(Picha
na Mwamvua Mwinyi )
Eneo
la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji
(Stiegler’s Gorge Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts
2,100 za umeme,linavyoonekana .
Mkuu
wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Mloka kilicho karibu na pori la akiba la Selou .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,na ujumbe wake wakikagua eneo la mto huo.(Picha na Mwamvua Mwinyi )
Na Mwamvua Mwinyi ,Rufiji
Wakazi
wa wilaya ya Rufiji ,Mkoani Pwani pamoja na watanzania kijumla
wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika
maporomoko ya mto Rufiji (stiegler’s gorge hydropower dam project),ambao
utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 .
Mradi huo utazalishwa kutoka chanzo hicho , katika pori la akiba la Selou Kanda ya Kaskazini (Matambwe ).Kwasasa
nchi inazalisha megawatts 1,450 lakini Stiegler’s gorge itazalisha
megawatts 2,100 hali itakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi .
Akizungumza
mara baada ya kwenda kukagua na kujiridhisha eneo utakapozalishwa mradi
huo kabla ya utekelezaji kuanza,Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist
Ndikilo, alisema tangazo rasmi limeshatolewa na wizara ya nishati na
madini tangu august 30 mwaka huu.
Aidha alifafanua ,tangazo hilo linawapa nafasi kwa makampuni ya ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme .Mhandisi Ndikilo,alibainisha kampuni yoyote iwe ya ndani ama nje ya nchi ikikidhidhi vigezo itatangazwa .
Alieleza endapo mradi utakamilika utawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika na kuvutia wawekezaji kwa wingi.Mhandisi
Ndikilo ,alisema wilaya ya Kisarawe na baadhi ya maeneo ya wilaya ya
Kibiti na Rufiji umeme ukatikakatika hivyo kuna changamoto ya upungufu
wa umeme hali inayokwamisha jitihada za kuinua sekta ya uwekezaji na
viwanda .
“Tatizo
la umeme bado ni kubwa mkoani hapa licha ya mkoa huu kusheheni viwanda
“Mradi umekuja muda muafaka ambapo mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa
viwanda ” alifafanua .
Faida
moja wapo ya mradi ni kuwa na maji mengi ya kunywa na viwandani kwa
mikoa ya Pwani ,Dar es salaam na Morogoro ,utaliii ,maji kwa ajili ya
wanyama pori na kilimo .
Mhandisi
Ndikilo alieleza ,mradi umekuja muda muafaka na umefika mahala pake
,ambapo Mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda .“Ni
nia ya serikali ya awamu ya tano kuhakikisha mawazo ya baba wa taifa
hayati mwl .Julius Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya kuzalisha umeme
kutoka katika maporomoko ya mto huo yanatekelezwa kwa haraka
iwezekanavyo “alisema mhandisi Ndikilo .
Baada
ya kutembelea eneo la mradi mhandisi Ndikilo ,alipata fursa ya kwenda
kuzungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho mpakani na pori la
akiba la Selou .Mhandisi Ndikilo, alisema ujenzi wa mradi huo utafungua milango ya kiuchumi na ujasiriamali na kibiashara .
Kwa upande wa wakazi wa Mloka ,Ikwiriri na Kibiti waliliridhia na kuonyesha kukubali maendeleo wanayosogezewa .Mkazi wa Mloka ,mzee Mbonde ,alisema alikuwepo enzi za hayati baba wa taifa mradi ulipofanyiwa tathmini na wa Norway.
Mzee Mbonde na bibi Fatuma Majengo walimpongeza mh rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kwa kubeba mzigo .Walisema kwa mwanzo huu ,Dk.Magufuli atatatua tatizo la uhaba wa umeme.
Eneo
litakalotumika kujenga mradi ni kilometa za mraba 1,350 ambalo ni sawa
na asilimia tatu pekee ya eneo lote la pori la akiba la Selou yenye
ukubwa wa km za mraba 50,000 .
Mkuu
wa pori hilo la akiba la Selou kanda ya kaskazini (Matambwe)Lawrence
Okode ,alisema katika historia jina la Stiegler’s gorge limetokana na
mjerumani aliyefariki katika eneo hilo aliyejulikana kwa jina la
Stiegler’s baada ya boti yake kugonga jiwe kubwa na kusababisha umauti
wake .