Afisa afya wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na viongozi wa vijiji wa tarafa ya pawaga kuhusu uboreshaji wa vyoo bora kwa lengo la kutatua tatizo la ugonjwa wa kipindupindu ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika tarafa hiyo walianza kutoa elimu kwa viongozi wote na baadae wakahamia kwa wananchi.
Afisa afya wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na mama moja ambaye hana choo bora na kutundikiwa bendera ilikuwa inamuonyesha kuwa hana choo bora katika kijiji cha mboliboli tarafa ya pawaga mkoani Iringa.
Afisa afya wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akisimamia zoezi la utundikaji wa bendera kwa wasio na vyoo bora
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Halmashauri ya wilaya ya
Iringa imetumia shilingi milioni mia
moja na tisini (190,000,000 ) kupambana na tatizo la milipuko ya ugonjwa wa
kipindupindu katika tarafa ya pawaga na Idodi mkoani Iringa na ni miongoni mwa
halmashauri 156 zinazotekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira
Tanzania bara.
Akizungumza wakati wa utoaji
elimu ya matumizi ya vyoo bora katika tarafa ya pawaga afisa afya wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya
aliwataka wananchi kuanza kutumia vyoo bora ili kumaliza tatizo la milipuko
ya ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa ukiwakumba mara kwa mara.
“Jamani chanzo mmoja wapo
cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ni matumizi ya vyoo ambavyo sio bora
hivyo mnatakiwa kutumia vyoo bora na kutoa elimu kwa wananchi wenu maana nyinyi
ndi wenye wananchi na leo tunawapa hii elimu nyie viongozi tunaomba muifikishe
elimu kwa wananchi”alisema Nkya
Nkya alisema walitoa elimu
ya uboreshaji wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka
kwa sabuni mara ya kutoka chooni kwa ngazi ya kaya na shule za msingi na
sekondari,Vyuo,taasisi za kidini,taasisi binafsi,taasisi za kiserikali kama
ofisi za serikali na vituo vya afya lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa
wa kipindupindu.
“Ukiangalia hadi sana
tumefanikiwa kuzifikia jumla ya kaya 24 zilizotekeleza kampeni hiikupitia wadau
mbalimbali kama wizara ya afya,wizara ya maji,wizara ya elimu
(RWSSP),halmashauri ya wilaya ya Iringa,UNICEFU,SNV na WARID na jumla ya kata nne ambazo ni
ilolompya,Mlenge,Mboliboli na Itunundu zimeanza kutekeleza rasmi kampeni hii
kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018” alisema Nkya
Mwezi wa pili hadi mwezi wan
ne mwaka 2016 ndio kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika
halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo kata za Mboliboli na Mlenge zilikumbwa
na ugonjwa huo huku vijiji vya Luganga,Mnadani,Idodi na Mafuruto vilikuwa na
idadi ndogo ya wagonjwa wa kipindupindu.
Aidha Nkya alisema kuwa
mikakati ya halmashauri ya wilaya ya Iringa kuzitambua kaya na taasisi zisizo
na vyoo bora,kutambua vibarua na wamiliki wa mshamba ya mpunga,kufanya ukaguzi
wa mara kwa mara wa usafi wa mazingira vijijini na kutoa elimu ya usafi wa
mazingira kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kisitokee tena
katika halmashauri hiyo.
“Tumepeana maagizo ya
kutekeleza kama kuwawekea bendera nyekundu kaya na taasisi zote ambazo hazina
vyoo bora,kutoa muda maalumu wa kuboresha vyoo vyao vinginevyo kuna faini
ambayo itatolewa kwa kaya na taasisi ambazo zitakuwa hazijaboresha vyoo vyao”
alisema Nkya
Nyamiki Kimsau ni mwananchi
wa kijiji cha Usolanga pawaga alisema kuwa kuwa ugonjwa kipindupindu umekuwa
sugu katika kijiji hicho kutokana na wananchi wemgi kutokuwa na vyoo bora
ambavyo vinakidhi kuishi na afya bora.
“Wananchi tukiwa tunafanya
usafi na kuwa na vyoo bora basi tunaweza kuepukana na milipuko ya ugonjwa wa
kipindupindu hivyo naomba serikali kuwa wakali kwenye swala la kuwa na vyoo
bora ili kuondokana na aibu ambayo imekuwa inatutafuna kwa muda sasa” alisema
Kimsau
Naye Mwaita Bin jumbe
alisema kuwa kweli wananchi wa kijiji cha mboliboli hawana vyoo bora kutokana
na ugumu wa maisha hivyo wanaomba kupewa muda ili waweze kuboresha vyoo bora
lakini swala la ugonjwa wa kipindupindu bado unawakumba kila mara.
“Jamani tunaomba viongozi
mtoe elimu ya kutosha kwa wananchi ili wajue umuhimu wa kuwa na vyoo bora
tofauti na hali iliyopo hivi sasa” alisema Bin jumbe
Hamis Matyame ni kijana wa
kijiji cha mboliboli aliita serikali ya kijiji kutafuta njia mbadala ya
kuwachimbia vyoo bora wazee ambao hawana uwezo wa kifedha na guvu kazi kwa
sababu wasipo saidiwa ugonjwa wa kipindupindu hauta koma katika tarafa ya
pawaga.
“Mimi kama kijana napenda
kuwasaidia wazee kuboresha vyoo ila hapa kijijini kuna wazee wengi hivyo pekee
yangu siwezi hivyo naiomba serikali kutafuta njia mbadala kuwasaidia hawa wazee”
alisema Matyame
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia