MAMIA WAMIMINIKA KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA (WCF) IKIWA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI JENISTA MHAGAMA


Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na kulipa michango

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema.
Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.
“Kwakweli tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema Bw. Luvena
K-VIS Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza  ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF  kujisajili na kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.
 Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF

 Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe, (kulia), akimkabidhi cheti cha usajili Bw.Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refregerator ya jijini Dar es Salaam.
 Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kushoto), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko
 Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, akimsikiliza Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma
  Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, (kushoto), akimuhudumia Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe,(kushoto), akimuhudumia Bw. Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refrigeration, ya jijini Dar es Salaam.
 Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwasikiliza waajiri waliofika  ili kupatiwa huduma ya usajili na uwasilishaji michango katika Mfuko huo.
 Maafisa wa WCF (kulia), wakimsikiliza Mama huyu mwajiri aliyefika kupatiwa huduma.



Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post